Napoli Kutangaza Ubingwa Leo Wakishinda

Klabu ya Napoli inayoshiriki ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A wanaweza kutangaza ubingwa leo endapo watashinda mchezo wake dhidi ya klabu ya Salernitana mchezo utakaopigwa katika dimba la Diego Maradona.

Napoli wamekua na msimu bora kabisa ambapo wakishinda leo watakua wamefikisha alama 81 ambazo zitakua haziwezi kufikiwa na mpinzani yeyote katika ligi kutokana na michezo iliyobakia, Hivo klabu hiyo inatarajia kupata ubingwa wake wa tatu katika historia ya klabu hiyo.napoliVijana wa Luciano Spalletti wamepata utelezi zaidi katika kuelekea kutangaza ubingwa wao kwani wapinzani wao waliokua wanakamata nafasi ya pili katika ligi hiyo klabu ya Lazio wamepoteza mchezo wao mapema leo dhidi ya klabu ya Inter Milan kwa mabao matatu kwa moja.

Napoli wakifanikiwa kushinda leo watakua wanatangaza ubingwa wa ligi hiyo wakiwa na michezo nane mkononi, Kwani leo wanacheza mchezo wao 32 dhidi ya Salernitana hivo hii ni rekodi pia wanaiweka klabu hiyo kutoka mitaa ya Naples nchini Italia katika kuthibitisha klabu hiyo ilikua kwenye msimu wake bora kabisa walifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya kwa mara ya kwanza kwenye historia ya klabu hiyo.napoliKlabu ya Napoli endapo itatangaza ubingwa wa ligi kuu ya Italia leo utakua ni ubingwa wao wa tatu katika historia ya klabu hiyo, Inakua imepita miaka 33 tangu klabu hiyo ishinde taji hilo mwaka 1990 wakiwa na gwiji wa kimataifa wa Argentina Diego Armando Maradona.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.