Neymar: Tujihadhari na Korona, Tubaki Nyumani

Mchezaji wa Soka la kulipwa mwenye asili ya ki Brazili anaecheza katika ligi kuu ya Ufaransa maarufu kama league 1 katika timu ya Paris Saint-Germain Neymar Da Silva Santos Junior ametikisa vichwa vya habari duniani kote mapema leo baada ya kutangaza kuchangia yuro laki saba na sabini 770,000 kwa Shirika la Afya Duniani na taasisi rasmi ya kuchangia pesa za kupambana na virusi vya Korona (Covid19) iliyo undwa na watu maarufu nchini Brazil.

Kujitolea huko kwa Neymar kumetangazwa leo hii na chombo cha habari cha Brazili kwenye kipindi cha Fofocalizando “pesa alizo changia Neymar zinaenda kusaidia waathilika wa gonjwa hili na kwenda kusaidia wale wote wasiojiweza hususan kwenye kipindi cha zuio la kubaki nyumbani kwa wananchi wote lililotolewa kwenye nchi tofauti tofauti za Duniani” Alisema mtangazaji wa kituo hicho.

Wiki kadhaa zilizopita Neymar alipost kwenye kurasa wake wa mtandao wa Instagram video fupi iliyo onesha akipiga makofi kama ishara ya kuwashukuru wahudumu wa Afya kujitolea na kuhatarisha maisha yao katika kupambana na Corona, Huku chini ya video hiyo kukiwa na msisitizo wa kuwahusia wafuasi wake kubaki nyumbani na kujihadhari  na korona

Wanamichezo duniani kote wameonesha kuchangia pesa kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa korona. Wachezaji wa Barcelona mwezi uliopita walikatwa asilimia 70 ya mishahara yao wakati wiki hii kocha mkuu  wa timu ya  Brighton Graham Potter anekua ni kocha wa pili katika ligi kuu ya Uingeleza kujitolea kukatwa mshahara wake baada ya kocha wa Bournermouth Eddie Howe kufanya hivyo.

Alhamisi hii Waziri wa Afya nchini Uingeleza Matt Hancock amewataka wachezaji wa ligi kuu kukubali kikatwa mishahara yao ili kuounguzia mzigo wale wafanya kazi wasio cheza mpira kwenye timu zao.

 

3 Komentara

    Kweli kabisa

    Jibu

    Asante sana

    Jibu

    Nzuri kujikinga

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.