Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane anaripotiwa kuwa tayari ameshambainisha mshambulio wa Liverpool Sadio Mane kama kipaumbele namba moja cha klabu kwenye dirisha la uhamisho la Msimu wa joto.
Ikumbukwe kuwa Zinedine Zidane amerejea klabuni hapo kama meneja kwa mara ya pili na wala hahitaji kufanya makosa zaidi ya kukiboresha kikosi chake ili aweze kurejesha heshima ya klabu hiyo.
Staa huyu, Mane, amekuwa kwenye fomu nzuri ya kuchapa magoli katika msimu huu akiwa amewafungia Liverpool magoli 20 kwa michuano yote msimu huu. huku magoli 11 yakiwa yamepatikana katika gemu zake 11 za hapa karibuni.

Baada ya kurejea kwa meneja Zidane, Real Madrid wanaripotiwa kuwa wamerejesha majeshi na kumfanya mshambuliaji huyu kama kipaumbele. Real wanapania kuingia sokoni kuboresha kikosi baada ya kuwa na msimu mbaya.
Bila shaka Liverpool watakuwa wagumu kumuuza Sadio Mane, mmoja kati ya wachezaji wao muhimu kabisa klabuni hapo, huenda watajifikiria sana kufanya hivyo na kukubali kama dili litakuwa linalipa wakiwa na uhakika wa kuziba pengo lake.


Povel
Habar njema
Furahav
Iko vizuri.