Mchezaji wa zamani wa Barcelona anasubiria tena kusomwa kwa kesi yake baada ya kukamatwa tarehe 6 mwezi machi mwaka huu kwa kosa la kufoji hati ya kusafiria na kuingia nayo nchini Paragwai.
Ronaldo De Assis Moreira maarufu kama Romaldinho Gaucho aliyezaliwa mwezi wa tatu tarehe ishirini na moja huko Porto Alegre jijini Rio nchini Brazili amewahi kuitumikia timu ya taifa ya brazili na mpaka amepatwa na mkasa huo Ronaldinho alikua ni Barozi wa Barcelona. Katika uchezaji wake Gaucho alihudumu kwa uwezo mkubwa sana nafasi ya kiungo mshambuliaji lakini kunawakati alitumika kama mshambuliaji wa pembeni.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania ambae alishawahi kukumbatia taji la Kombe la dunia akiwa na timu ya taifa ya Brazili mwaka 2002, alikamatwa yeye na kaka yake Roberto nchini Paragwai kwa kosa la kuingia nchini humo kwa hati feki ya kusafiria. Hata hivyo Ronaldinho ameachiwa huru na hii ni baada ya kaka ambae pia ndio msimamizi wake kibiashara kukubali kulipa Dhamana ya dola za marekani milioni 1.6.

Jaji wa kesi hiyo amewaruhusu Ronaldnho na kaka yake kukaa kwenye hoteli ya Palmaroga kwa kipindi ambacho watakua wanasubiri kesi yao kusomwa tena huku garama ya dola laki 8 kwa kila mmoja wao ikitumika kama dhamana na wataruhusiwa kupokea wageni.
“kwa damana kubwa kiasi hiki itawafanya wasiweze kutoroka katika kipindi hiki cha kusubiri kesi kusomwa tena” alisema jaji Gustavo Amarilla
mchezaji huyo wa zamani wa Gremio, Flamengo na Paris Saint Germain ambae mara ya mwisho alicheza kimataifa mwaka 2015 na kutajwa kua mchezaji bora wa dunia mwanzoni mwa Karne hii.
mchezaji huyo mwenye miaka 40 kwa sasa alishawahi kua mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2004 na 2005 na kushinda kombe la dunia mwaka 2002 lakini pia ubingwa wa klabu bingwa ulaya akiwa na Barcelona.


Amiri Kayera
Dah kesi iishe apunzike maan dah
Franky
Good news