Klabu ya Fc Barcelona iko mbioni kumuongezea mkataba kijana mdogo ndani ya klabu hiyo Alejandro Balde ambaye amepandishwa kutoka timu ya vijana ya klabu hiyo.

Alejandro Blade mwenye umri wa miaka 22 amabye amepandishwa kutoka timu ya vijana ya klabu hiyo amekua akionesha uwezo mkubwa tangu aanze kupata mafasi ya kucheza klabu hapo chini ya kocha Xavi.BarcelonaKijana Balde ambaye pia alipata nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kilichoshiriki michuano ya kombe la dunia nchini Qatar chini ya kocha Luis Enrique, Na hiyo ilitokana na kiwango bora ambacho alionesha ndani ya klabu yake.

Klabu ya Barcelona wamefikia hatua nzuri na mchezaji huyo katika kumuongezea mkataba baada ya kuonekana pande zote mbili zinahitaji kuona dili hilo linafanikiwa, Hivo ni wazi kijana huyo atamwaga wino wa kuendelea kusalia kwenye viunga vya Camp Nou.BarcelonaKlabu ya Barcelona wanamuona Alejandro Balde kama mbadala wa muda mrefu wa beki wao wa kushoto aliekaa klabuni hapo kwa muda mrefu na kucheza kwa mafanikio Jordi Alba, Hivo kutokana na umri wa Balde ni wazi kama ataendelea kua kwenye ubora huu basi atawasidia miamba hiyo ya Blaugrana kwa muda mrefu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa