Mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal anayekipiga kwenye klabu ya Liverpool Sadio Mane anajiandaa kufanyiwa vipimo na klabu ya Bayern Munich baada ta kufikiana makubaliano na klabu ya Liverpool.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Southmpton alitangaza nia yake ya kutaka kuondoka klabuni hapo msimu huu, baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka sita sasa, Barcelona na Real Madrid zilionesha nia ya kuhitaji huduma yake ingawa hawakutuma maombi rasmi.

Bayern Munich

Bayern Munich waliwasilisha offer mara mbili za kuhitaji huduma yake, klabu ya Liverpool ilizikataa offer hizo, klabu ya liverpool imekubali offer ya kiasi cha £40m ikiwa na nyongeza ya kiasi £15m kutoka kwenye offer za awali, huku wakifanikisha usajiri wa Darwin Nunez.

Sadio Mané siku ya leo amekutana uongozi wa klabu ya liverpool ili kuweka mambo sawa, baada ya kufanya kikao na viongozi wa klabu ya Bayern munich ambapo walikuwa na kikao kuhusu makubaliano binafsi ya mshahara.

Sadio Mané akiwa na klabu ya Liverpool amefanikiwa kushinda makombe sita, Premier League 1, FA Cup 1, Carabao Cup 1, UEFA Champion League 1,UEFA Super Cup 1 na FIFA world cup 1 pia amekuwa mfungaji bora wa Uingereza mara moja.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa