Klabu ya RB Leipzig imekamilisha usajili wa kudumu kwa kiungo Xaver Schlager kutoka Wolsburg dili itakayodumu mpaka 2026.

Kwa mujibu wa Kicker na Sky Germany waliripoti siku ya Alhamisi kwamba pande zote zipo kwenye majadiliano wakiwa katika hatua nzuri kukamilisha dili ya €12m

Schlager alitua Wolfsburg akitokea RB Salzburg kwa kitita cha euro milioni 15 mwaka 2019 na alikuwa amesaliwa na mwaka mmoja kwenye mkataba wake.

Schlager ametua Leipzig kuboresha eneo la kiungo akichukua nafasi ya kati ya Tyler Adams au Amadou Haidara ambapo mmoja kati yao lazima aondoke.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Austria mwenye umri wa miaka 24 alicheza dakika 1048 kwenye michezo 14 ya Bundesliga msimu uliyopita lakini alikuwa akipambana na majeraha.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa