Mchezaji wa Azam FC Prince Dube ameibuka mchezaji bora wa mwezi mei wa VPL, huku kocha wake mzambia George Lwandamina akiibuka kocha bora wa mwezi mei vilevile kufuatia mchezo mzuri walioonesha katika mwezi huo.

Katika mechi tano za mwisho Azam ilizocheza imefanikiwa kushinda mechi nne kati ya tano na kufanikiwa kukusanya alama 13 kati ya 15. Price Dube akifikisha jumla ya magoli 14 na kuwa kinara wa wafungaji wa VPL.

Lwandamina toka achukue Azam amekuwa akifanya mambo makubwa na kuipa timu uwezo wa kuwa na mchezo endelevu ambao ni mzuri kitendo cha kuihakikishia Azam kubaki nafasi ya tatu ya msimamo.

Azam wanaingia kwenye mbio za kuwania ubingwa sawa na Simba na Yanga kwa uchezaji mzuri wa Dube pamoja na muongozo imara wa Lwandamina akiwa kama kocha wa wanalambalamba hao wa Chamazi.

WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa