Laguna Larga ndio sehemu ambako Mwamba Dyabala amezaliwa na kukulia na mara kwa mara tunakutana na nyakati ngumu katika maisha, wala hatupaswi kuzikimbia bali kuzikabili na kuzishinda. Hii sio kwenye mpira pekee bali kwenye maisha yetu kiujumla. Vitu vibaya hutokea lakini tunapaswa kusonga mbele. Huo ndio mzunguko wa maisha
Kama maisha ya shida niliyopitia wakati nakua kule kwetu Laguna Larga. Maisha ya wananchi wengi hayana uhakika wa kesho iliyo bora. Mji wenye majambazi sugu wa kupora kwenye mabenki. Kama ambavyo nilivyompoteza baba yangu nikiwa na miaka 15. Maumivu yasiyo elezeka
Aliwekeza kila kitu kwenye soka langu. Nilitamani aje kufurahia matunda ya kipaji cha mwanae. Kifo chake kilifanya nipoteze maana ya kucheza soka. Nilifikiria kuacha kabisa. Lakini katika magumu yote hayo sikupoteza tumaini
Leo hii nafurahia kucheza soka katika kilabu kikubwa Italia. Lakini sijamsahau baba yangu. Kila goli ninalofunga basi ni kwa ajili yake, kwa sababu najua ananitazama. Pia nikifunga huwa naonesha ishara ya mask (Dybala Mask)
Ni mask ya Gladiator. Kwamba tunapokuwa kwenye nyakati ngumu, tunapaswa kuvaa mask zetu za kishujaa ili kutupa nguvu pasipo kupoteza tabasamu na ukarimu wetu. Kama ambavyo anafanya Maximus kwenye filamu ya Gladiator
Katika ushangiliaji wa magoli yangu, ndani yake nataka kufikisha ujumbe kwa dunia. Hatupaswi kukata tamaa. Tuwe kama Gladiator, vaa mask endelea kupambana
Ladies and Gentlemen, that’s Paulo Dybala La Joya (The Jewel). Fundi mmoja kwenye uzi wa Juventus. Pengine angekata tamaa dunia isingefaidi ufundi wa soka lake
Ukifika Laguna Larga usianze jina la Lionel Messi halafu ndio utaje Dybala, hawatakuelewa. Kwao, Messi ni namba mbili jana, leo, kesho na siku zote. Namba moja ni kipenzi chao Paulo wala si mwingine
Katika eneo la Ruta Nueve wameweka bango kwenye barabara kuu inayounganisha Cordoba, Rosario na Buenos Aires. Bango linasomeka HUU NI MJI WA PAULO DYBALA
Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.
Dube yuko vizur namkubali sana