Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Afisa Mkuu mtendaji wa Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi anasema mabingwa hao wa Ufaransa hawatamuuza mshambuliaji wao Kylian Mbappe, 22.

Aston Villa wako tayari kumnunua kiungo wa kati wa Southampton na England James Ward-Prowse, 26, siku moja baada ya kukubali kuvunja rekodi ya usajili wa klabu hiyo kumsaini kiungo wa kati mwenzake Emiliano Buendia kutoka Norwich.

Tetesi zinasema, Itagharimu euro milioni 200 sawa na (paundi milioni 171.8) kumnunua mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 20, kutoka Borussia Dortmund msimu huu.

 

Erling Haaland

Tetesi zinasema, Wolves wanajiandaa kupokea ofa ya Arsenal wiki hii kuhusiana na kiungo wa kati wa Ureno Ruben Neves, 24.

Barcelona wamefufua tena mpango wa kumsaka mlinzi wa Manchester City Mhispani Aymeric Laporte, 27, na huenda wakamtoa Sergi Roberto, 29, kama sehemu ya kufanikisha mkataba.

Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 34, bado huenda akajiunga na AC Milan, licha ya Chelsea kutangaza mpango wa kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja wiki iliopita.

Barcelona wameamua kutoongeza ofa ya Georginio Wijnaldum, 30, baada ya Paris St-Germain kuongeza mara mbili marupurupu ya ofa iliyotolewa na Barca. Kiungo huyo wa kati wa Uholanzi, ambaye yuko huru kuondoka Liverpool,anajiandaa kusaini mkataba wa miaka mitatu na PSG.

Juventus huenda wakajaribu hatua sawa na hiyo na mchezaji mwingine wa anayelengwa na Barcelona, mshambuliaji wa Uholanzi Memphis Depay, 27, ambaye anajiandaa kuondoka Lyon kwa uhamisho wa bure.

 

Depay: Naweza Kubaki Lyon Mpaka Mwisho wa Msimu.
Memphis Depay

Tetesi zinasema, Real Betis wamepiga hatua katika mazungumzo yao na mlinzi wa Paraguay Fabian Balbuena, 29, ambaye mkataba wake katika klabu ya West Ham inaelekea kumalizika.

Tottenham itathibitisha uteuzi wa mkufunzi wa zamani wa Juventus Fabio Paratici msimu huu, baada ya juhudi zao za kumpata mkufunzi wa zamani wa-Juve na Inter Milan Antonio Conte kugonga mwamba.

Tetesi zinasema, Lazio huenda wakamsajili meneja wa zamani wa Juventus na Chelsea Maurizio Sarri, 62, kama mkufunzi wao mpya wiki hii.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

3 Komentara

  Nice update

  Jibu

  Tetesi safi

  Jibu

  Safi

  Jibu

Acha ujumbe