Klabu ya Yanga imekamilisha usajiri wa kiungo wa kimataifa kutoka Burundi Gael Bigirimamana ambaye pia alishawai kuichezea timu ya taifa ya Uingereza chini ya miaka 20 mwaka 2013.

Gael Bigirimamana alizaliwa nchini burundi ambapo baba yake ndio mwenye asili ya burundi, huku mama yake akiwa na urai wa Rwanda, familia ya mzee Bigirimamana walihamia nchini Uingereza mwaka 2004 kama wakimbizi wa vita vya wenye kwa wenyewe nchini Burundi.

Gael Bigirimamana, Gael Bigirimamana Kiungo Mpya wa Yanga, Meridianbet

kipaji cha Gael Bigirimamana kilianza kuoneka kwenye klabu ya Coventry City, ambapo mwaka 2011 alifanikiwa kuanza rasmi kucheza soka la kulipwa kabla ya kusajiriwa na klabu ya Newcastle United mwaka 2012.

Mpaka sasa Bigirimamana amevichezea vilabu saba barani ambavyo ni Newcastle United, Rangers, Mothewell, Hibernian, Solihull Moors Glentoran na Coventry City ambapo alisajiriwa mara tatu kwa vipindi tofauti.

Yanga ndio klabu pekee na ya kwanza kumleta Bigirimamana Afrika baada ya kuishi barani Ulaya kwa muda wa miaka kumi na moja kwenye maisha yake ya soka.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa