Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes Da Rosa, amefunguka kuwa moja ya malengo yake kwa sasa ni kuhakikisha wanapata matokeo katika kila mchezo wa ligi, ukiwemo mchezo wao ujao dhidi ya Namungo baada ya kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba inarejea tena kwenye Ligi baada ya safari ya kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye hatua ya robo fainali ambapo, leo Jumamosi watakuwa uwanjani kucheza dhidi ya Namungo mkoani Lindi.

Timu hiyo ambayo inaongoza ligi kwa pointi 61 sawa na Yanga, inayokamata nafasi ya pili lakini wakiwa na tofauti ya mabao na mechi (Yanga wako mbele kwa mechi nne).

Gomes amesema kuwa kwa sasa watawekeza nguvu zao zote katika mechi zao za Ligi kwa kuanza na Namungo kwa kuwa wanataka kuona wanafanikiwa kutetea ubingwa wao kufuatia kuondolewa kwenye michuano ya kimataifa.

gomes

“Kitu pekee kwa sasa ni kujipanga upya kwa ajili ya msimu ujao ili tuone kwa namna gani tunaweza kufika mbali ya tulipoishia, nguvu yetu tunaipeleka kwenye mechi zetu za ligi kwa kuhakikisha tunashinda, tukianzia mechi yetu dhidi na Namungo, maana ndiyo itakuwa ya kwanza katika ligi.

“Unajua mashindano si rahisi wala si timu ya kawaida kwa kuwa kila timu inakuwa imejiandaa kupambana kwa kuhakikisha wanapata matokeo, hivyo tunaenda kucheza ugenini tukiwa na lengo moja pekee la kuhakikisha tunashinda ili kujiweka kwenye wakati mzuri wa kutetea ubingwa wetu msimu huu,” amesema Gomes.


BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa