Tetesi zinasema, Manchester City wanajiandaa kumuuza mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 26, msimu huu baada ya kuwa naye kwa miaka sita.

Erling Braut Haaland, 20, wa Borussia Dortmund amesema anaheshimu mkataba wake katika hatua ambayo inaashiria mshambuliaji huyo wa Norway hana mpango wa kuhama klabu hiyo msimu huu wa joto.

Barcelona wana imani watakamilisha mchakato wa kumsajili mshambulizi wa Manchester City na Argentina Sergio Aguero, 32, pamoja na kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, kwa uhamisho wa bila malipo hivi karibuni. Mikataba ya wachezaji hao wawili inakamilika wa joto.

 

Wakala wa Paul Pogba Ndani ya Turin!

Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 28, anaonekana kuwa ndoto ya usajili kwa Juventus.

Tetesi zinasema Meneja wa Chelsea Thomas Tuchel yuko tayari kusalia Blues kwa kusaini mkataba mpya. Mjerumani huyo aliye na umri wa miaka 47 amesalia na mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa.

Tetesi zinasema, Ajax wanataka kumsajili winga wa Tottenham Hotspur na Uholanzi Steven Bergwijn, 23.

Liverpool inaweza kukusanya £80m kwa kuwauza wachezaji wanane msimu huu dirisha la uhamisho litakapofunguliwa. Wachezaji hao ni pamoja kiungo wa Uswizi Xherdan Shaqiri, 29, mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi, 26, na mshambuliaji wa Japan Takumi Minamino, 26.

Tetesi zinasema Aston Villa wanataka kumsajili winga wa Burnley na England Dwight McNeil, 21, na mshambuliaji wa Norwich City Muargentina Emiliano Buendia, 24.

 

Tetesi zinasema, kiungo wa kati wa zamani wa Chelsea Oscar, 29, anataka kurejea Stamford Bridge mika minne baada ya mchezaji nyota huyo wa Brazili kuhamia klabu ya China ya Shanghai Port.

Mchezaji wa Real Madrid Raphael Varane,28, anayehusishwa na uhamisho wa kwenda Manchester United, anasisitiza kwamba kipaumbele chake ni Ufarasa na mashindano ya Ulaya na wala sio mazungumzo ya uhamisho.

West Ham United wamemwambia mchezaji wa safu ya kati na nyuma wa Paraguay Fabian Balbuena, 29, kwamba yuko huru kuhamia klabu yoyote mkataba wake utakapokamilika mwisho wa mwezi Juni.


BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa