2019 imekuwa ya kipekee sana kwa mashabiki wa WWE duniani kote huku yakishuhudiwa mapambano makubwa na ya aina yake. Mbali na mashindano hayo kuendelea pia, suala la nyota wanaoshiriki mchezo huo kuangalia sehemu ambazo zitawafaa wao kujiunga na makampuni mengine mengi yatakayowafaa hapo baadaye lilikuwepo.
Kama ilivyo kwa kila mwanamichezo huangalia upande wenye maslahi na kama mfumo wake unaweza kuwa rafiki kwake kuendelea kuhudumu upande wa kampuni fulani ambalo lina mifumo salama kwake. Leo tunakuletea majina ya nyota wa muda mrefu ndani ya ulingo ambao hawategemewi kabisa kuzisaliti pande walizopo:
Triple H, mkongwe wa mchezo huo akiwa na historia ya aina yake kwa kila mpinzani aliyepata nafasi ya kukutana naye. Kwake WWE ni kama nyumbani na hawezi kabisa kushuka kushindana aina nyingine ya mashindano. Yeye ni kiongozi mkubwa katika kampuni ya NXT ambayo ina heshima kubwa ya kukuza washindani wengi na kuwalea. Hivyo hatuwezi kutegemea nyota huyo kusaliti chama chake hicho.
Roman Reigns, aliachana na mchezo huo 2018 baada ya kutwaa ubingwa wa kidunia akiwa na historia kubwa sana aliyoijenga. Kwa sasa anapambana na maradhi ya Leukemia japo hata umri wake haumruhusu kurudi ulingoni tena. Endapo akirejea atabakia kama nyota wa WWE ambako wao ni kama picha halisi ya kampuni na wanafanya makubwa kutangaza zaidi kampuni hilo.
John Cena, wengi wamembatiza kwa jina la “Loyalty” na amekuwa akilitumia sana ulingoni kwenye mashindano yake yote anayohusika. Mshindi huyo mara 16 wa michuano hiyo ataendelea kuonekana miaka yote akiwa chini ya WWE na sio kwingine. Hilo linatokana na uaminifu ambao kama kampuni limeujenga kwao na wao kuonekana kama sehemu ya mafanikio ya WWE.
Kane, mpiganaji mwenye heshima kubwa sana ambaye kwake sheria sio kitu akiwa ulingoni pamoja na vurugu zake zote bado ataendelea kuonekana uwanjani akiwa kama zao la WWE na ataendelea kuijengea heshima kampuni hiyo. Amekuwa na aina ya pekee ya kupigana ambapo haifanani na yeyote yule kati ya wapiganaji wa sasa. Nguvu, akili na kujiamini ni vitu ambavyo vimemfikisha hapo alipo kwa sasa.
The Undertaker, mtu mwenye jina kubwa ndani ya michuano hiyo akiwa chini ya WWE na wengi walimbatiza jina la Mr. WWE kutokana na uwezo wake akiwa ukingoni na utawala aliouonesha akiwa mpiganaji. Pamoja na uimara wake alipokea kichapo kutoka kwa Roman mwaka 2017 lakini atasalia kuwa upande wa WWE.
Fatina mfingi
Makala nzur