Hojlund Nje Wiki Mbili Tatu

Mshambulaiji wa klabu ya Manchester United ambaye amekua tegemezi sana klabuni hapo hivi karibuni Rasmus Hojlund amepata maejara ya misuli ambayo yanakadiriwa yatamuekea nje ya uwanja kwa takribani wiki mbili mpaka tatu.

Manchester United inaendelea kuandamwa na wimbi la majeraha msimu huu kwani wiki hii hii imetoka taarifa ya beki wa kushoto wa klabu hiyo Luke Shaw kua atoksekana kwenye timu hiyo kwa miezi kadhaa.hojlundMshambuliaji Hojlund ambaye ameanza kuonesha makali yake ndani ya timu hiyo baada ya kufunga katika michezo sita mfululizo ya ligi kuu ya Uingereza na kuweka rekodi, Amepata majeraha ambayo yataifanya timu yake kupitia kipindi kigumu.

Klabu hiyo kwasasa haina mshambuliaji asili aliye fiti kwani Anthony Martial anauguza majeraha mpaka sasa, Huku Rasmus nae amepata majeraha kwa namna moja ama nyingine ni hali ambayo inakwenda kumpasua kichwa kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag.hojlundTaarifa zinaeleza kua kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Fulham kocha Erik Ten Hag amepanga kumuanzisha kinda Omar Forson kama mshambuliaji ili kuziba nafasi ya Rasmus Hojlund ambaye amepata majeraha.

Acha ujumbe