Suala la kumuuza nyota Jude Bellingham kwa Borussia Dortmund ni kipengele, licha ya staa huyo kuhusishwa na vilabu vya Liverpool na Chelsea.
Dortmund wanaripotiwa kuwa hawapo tayari kumuuza Bellingham kiangazi kijacho, na wanajiandaa kuzikataa ofa zozote zitakazowasilishwa klabuni hapo za uhamisho wa staa huyo.
Nyota huyu wa miaka 18 amefanya vizuri msimu uliopita, akiwa amecheza mechi 46 na kuchangia magoli 46 katika michuano yote, akitoa asisti nne na kufunga magoli manne.
Msimu huu umeanzwa vyema pia na Jude Bellingham, ambaye tayari amefunga goli moja na kutoa asisti tatu kwenye mechi tano alizocheza.

Vilabu vya Chelsea na Liverpool, vyote vilikuwa vinahusishwa na nia ya kumsajili staa huyu.
Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa klabu ya Dortmund haina mpango wa kumuuza kinda huyu. Imeripotiwa kuwa staa huyu ameongezewa mara mbili ya mshahara wake wa awali aliposaini mkataba mpya mwishoni mwa mwezi Juni. Mkataba huu ambao unadumu hadi mwaka 2025 unamlipa takribanbi £100,000 kwa wiki.
Chelsea na Liverpool sio vilabu pekee kutoka EPL vinavyohusishwa na staa huyu, Man City na Manchester United pia wanahusishwa na Jude Bellingham.
Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.


