Khalid Aucho kiungo wa Yanga SC ni miongoni mwa wachezaji wa timu hiyo ambao wapo Mbeya kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo wa raudi ya 29 unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Aucho ndani ya Yanga SC amekuwa mhimili eneo la kiungo mkabaji ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi na katika mechi zilizopita, Khalid Aucho hakuwa fiti asilimka 100 baada ya kupata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union alipogotea dakika ya 44 na nafasi yake ikachukuliwa na kiungo Mudathir Yahya.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa sasa tayari amerejea katika ubora wake na anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaopata nafasi kucheza mchezo ujao wa mzunguko wa pili.

Yanga SC kwenye msimamo ni namba moja ikiwa na pointi 73 baada ya kucheza mechi 27 inakutana na Prisons ambayo imecheza mechi 28.
Tanzania Prisons ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 30 inapambana kujinasua kwenye nafasi ya kucheza play off.
Safu ya ushambuliaji ya Yanga SC imefunga mabao 71 ikisa ni timu namba moja kufunga mabao mengi huku Prisons safu ya ushambuliaji imetupia mabao 23.

