Mashindano ya Mbio, maarufu kama London Marathon ambayo yalikuwa yamesogezwa mbele kutokana na changamoto ya janga la virusi vya Corona yanatarajiwa kuwa yanaweza kuhusisha wanariadha wajuzi tu!
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa mashindano hayo Hugh Brasher, hii ni moja ya machaguo 10 waliyonayo mezani ambayo yanabadilika kila wakati na huenda yakapelekea kusogezwa mbele zaidi kwa mashindano haya.
Mashindano haya yalikuwa yafanyike Jumapili, lakini yalisogezwa mbele hadi Oktoba 4 kutokana na shida ya virusi vya Covid19.
Mwaka 2019, karibu wakimbiaji 43,000 walishiriki mbio hizi, huku Eliud Kipchonge na Kenenisa Bekele wakiwa tayarai kukutana na kuchuana vikali kwenye mbio za wanaume.

Brashier anasema kwa wana matumaini kuwa mashindano haya byatarejea mwezi Oktoba, lakini mpaka sasa bado haijafahamika nini hasa kinakwenda kutokea. Hivyo wanatarajia mabadiliko wakiwa wanatazama mazingira 10 ya uwezekano wa namna kufanya mashindano haya, na kunakuwa na mabadiliko ya mara kwa mara.
isha
Duuh corona ni ugojwa wa hatari sana maana umeharibu kila kila kitu