Tarehe 1/9/2013 Gareth Bale alitua rasmi Bernabeu kwa mkwanja mrefuu sanaa kama mavuno ya kilimo cha matikiti huko Dodoma, alikwenda kupata taabu za wanaume bila kujitambua.

Real Madrid ni timu ya kishua sanaa yaani ya kifalme wana style yao ya maisha , maana nyingine wanapendelea wachezaji wa kishua sana yaani wenye utajiri wa ubunifu uwanjani na uanamitindo kama Ramos , Marcelo , Zidane , Figo na wengine wengi..
Vichwani mwa kina mama na kina dada warembo wa Galaticos walijua kabisa jamaa hakua aina yao ila basi tu kuanzia sura mpaka aina ya uchezaji, iko ivo yaani hata Cloudio Makelele walijua sio style yao na walitema kama kina dada weupe wazuri wanavyoamini wahuni weupe sio style yao ila basi tu .

Katika mechi ya ligi kuu dhidi ya Espanyol 2015 Bale alikokota mpira kutoka winga ya kulia na kutafuta angle nzuri ya kufunga lakini akakosa huku Ronaldo akiwa katika nafasi nzuri ya kufunga basi Bernabeu iliibuka na kumzomea kila akishika mpira wahuni na warembo wa kifalme wanamzomea, huyu huyu aliyemwaga jasho na damu kuumaliza ukame wa kutopata UEFA zaidi ya miaka 10 hata leo hii hata akiingia sub anazomewa, anaonewa sanaa jamaa aliwaondoa City pale Bernabeu pia huyu huyu ndiye aliwavurugia usemi Liverpool pale Kyiv..
Gareth Bale anajua kabisa hawezi kuwaridhisha wale warembo royal sababu sura yake haiwavutii kama Ronaldo, anajua kukimbia tu na kupiga mashuti hawezi kupiga kanzu kama Zidane na Ronaldo , ndio maana hata wakimzomea anacheka.
Hata Zidane amekataa kabisa kumkubali Bale anamuona boya tu na ametamka wazi, huyu anakaunafiki Fulani maana alikua wa kwanza kuongea baada ya Cloudio Makelele kuuzwa na raisi pia inawezekana anajua class ya galaticos ndo maana anamtemaa waziwazi.
Bale amefanya makubwa sanaa pale Real amemwaga sana jasho na damu lakini ndo ivo wamekataa kumkubali ,watoto wa kiispanyola kina Isco Alarcon kuna muda wanayumba sanaa lakini wapi kina Vasquez ni homa za vipindi lakini nani anajali . Kikubwa hapa Gareth ameamua kuvaa miwani mweusi yupo tayari kwa lolote ndo maana akizomewa anacheka anajua Heshima yake ipo tu.


Furahav
Pambana mzee.