Nani angekubali kuiongoza Italy ile? Timu iliyosheheni mafundi wenye miguu yao, timu iliyosheheni vichaa vichwa vizima na bongo nusu. Ungezungumza nini mbele ya Franseco Totti, Danielle De Rossi na Gennaro Gatusso. Ila Cannavaro alikubali kuvaa kitambaa na bado akasimama kumpanga Marco Materazzi, Zambrotta na Fabio Grosso kwenye ukuta. Ilikuwa kazi ngumu zaidi ya kumnyang’anya gongo mlevi.
Ila Ugumu wa kazi, faida mwisho wa mwezi kwenye mshahara, alikuwa wa kwanza kunyanyua ndoo ya ubingwa wa dunia mwaka 2006 pale Ujerumani. Fabio Cannavaro mtoto wa mama mfanyakazi wa ndani na baba mhasibu wa benki. Alizaliwa Naples, akakulia Naples, kitabu cha maisha yake kilianza kuandikwa Naples.
Alianza kama mtoto muokota mipira pale Estadio San Paolo linapokipiga chama lake la nyumbani Napoli kabla ya baadae kujiunga na timu yao ya vijana. Akakua akiokota mipira huku akifurahia burudani kutoka kwa mchawi wa America Kusini Diego Maradona. Baadae alijiunga na timu ya vijana ya Napoli

Alianza maisha ya mpira kama kiungo mkabaji, baada ya kumtelezea Maradona siku moja kwenye mazoezi na kufanikiwa kumpora mpira kocha wake akamuhamisha na kumchezesha beki.
Alikipiga Napoli baadae akahamia Parma alipokutana na marafiki zake Gianluigi Buffon na Lillian Thuram kabla ya kujiunga na Inter Millan kwenye majira ya joto 2002.
Alijiunga na Juve mwaka 2004, hapa ndipo walipotengeneza ule ukuta wa Berlin ndani ya Turin. Fabio Cannavaro, GianLucca Zambrotta, Jenathan Zebbina na Federico Balzaretti, nafsi zile nne kwenye ukuta zingezuia hadi jua lisiwake licha washambuliaji waliozaliwa na binadamu.
Licha ya udogo wa umbo lake Cannavaro alikuwa hodari sana wa kucheza mipira ya vichwa, alikuwa hodari sana kupanga wenzake, alikuwa na uwezo wa kucheza beki yoyote. Kocha wa Inter Hector Cuper aliwahi kumchezesha full back zote, na bado akacheza kwa kiwango kilekile cha Cannavaro.
Ballon d’or ya 2006 inabaki na historia yake, tuzo pekee iliyotwaliwa na beki. Zingine zote zimebebwa na mastraika na viungo. Tuzo ya Fabio Cannavaro.


felister
beki kisiki aliyeishi maisha ya ushambuliaji
Issa
Canavaro beki pekee aliechukua ballion dior