Harry Maguire nahodha wa klabu ya Manchester United amewajibu waandishi wa habari ambao wanamuandika kila siku vibaya.

Mchezaji huyo ambaye amekua akishambuliwa zaidi na mashabiki wa klabu yake kutokana na kiwango ambacho amekua akikionesha ndani ya timu hiyo kutowafurahisha mashabiki wa klabu hiyo.

Maguire yeye ameonesha kutokusumbuliwa juu ya yale ambayo yanaandikwa na vyombo vya habari juu ya maoni ya mashabiki wa timu yake wanachokisema juu yake katika siku za karibuni ambacho mchezaji huyo amekua akicheza chini ya kiwango.

maguireBeki huyo amewajibu waandishi wa habari wanaoandika vibaya mitandaoni baada ya kusema “Watu wanapenda sana kuandika kuhusu mimi kwakua ni nahodha wa Manchester United, Hivo wanajua habari yao itauza zaidi”.

Harry aliendelea kwa kusema “Wanasahau nilienda kwenye michuano ya mataifa ya Ulaya nikiwa na majeraha ya wiki nane na bado niliingia kwenye timu bora ya mashindano”.

Kutokana maneno ya beki huyo anaonesha kuwajibu waandishi hao wanamuandika vibaya na kuonesha bado anaamini yeye ni bora na anastahili kupewa heshima anayostahili.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa