Winga wa Man City Riyad Mahrez na Raheem Sterling wanatajwa kuwekwa sokono kwa dirisha lijalo la uhamisho.

Licha ya kupata magoli 14 na asisti 12 kwenye michuano yote msimu huu, Raheem Sterling ameshindwa kuwepo kwenye vipaumbele vya Pep Guardiola, na anatarajiwa kuwa benchi kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Jumamosi hii.

Wakati huo, Mahrez  yeye alikanusha habari za kutemana na Man City kabla ya msimu ujao, lakini umri unamtupa mkono pia akiitafuta miaka 31 mwakani, basi ni wazi hatma yake City inaweza kuwa mashakani.

Man City: Sterling na Mahrez Sokoni
Man City: Sterling na Mahrez Sokoni

Kwa mujibu wa Daily Mail, Man City wako tayari kupokea ofa za wachezaji hawa wote ili waweze kupata pesa kwa ajili ya kumnasa nyota wa Aston Villa Jack Grealish.

Ripoti zingine zinasema kuwa Mikel Arteta anasaka kuwaunganisha tena wachezaji hao wawili pale Arsenal, lakini kutokana na changamoto za kiuchumi suala hilo linaweza kuwa gumu kidogo.


BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa