Klabu ya Manchester United imepanga kuingia sokoni kwenye dirisha la mwezi Januari kutafuta mshambuliaji baada ya kutangaza kuachana na mshambuliaji wake Cristiano Ronaldo siku ya jana.

Klabu ya Manchester United ambayo haikua na mpango wakuingia sokoni mwezi Januari lakini imelazimika kuingia sokoni kutafuta mshambuliaji mpya baada ya kuachana na staa huyo wa kimataifa wa Ureno. Staa huyo alikua anatumika chaguo la pili la kocha lakini ilikua inaongeza ubora kwenye kikosi hicho.manchester unitedHii imekuja pia baada ya klabu hiyo kuepuka kumlipa  mchezaji huyo kiasi cha paundi milioni 19 baada ya kumvunjia mkataba mchezaji huyo na gwiji huyo kukataa kulipwa, Imeifanya klabu hiyo kutunza hela hiyo na kuwafanya kufikiria kuingia sokoni dirisha dogo.

Mashetani wekundu ambao wamekua wakimtegemea Marcus Rashford na Anthony Martial kwenye safu ya ushambuliaji lakini muda mwingi Martial anakua kwenye majeraha hivo klabu hiyo wanahitaji kutafuta mbadala ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji.manchester unitedKlabu ya Manchester United inamtupia macho mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uholanzi na klabu Psv Eindhoven ambaye anafanya vizuri kwasasa inamtazama kama mbadala sahihi wa nyota Cristiano Ronaldo na anaweza kuimarisha safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa