Manchester United Yamuweka Lingard Sokoni

Baada ya kumalizana na Alexis Sanchez, sasa Manchester United wamehamia kwa Jesse Lingard. Ripoti zinasema, Man United wapotayari kusikiliza ofa ya timu yeyote inayomuhitaji mchezaji huyo [Lingard].

Lingard ambaye amekuwa na wakati mgumu katika kikosi cha Man United kwa muda sasa, muda wake kusalia katika kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer unahesabika. Kuchipukia kwa mshambuliaji machachari Mason Greenwood na mchakato wa kuisaka saini ya Jadon Sancho unaoendelea, ni dhahiri Lingard hana namba tena kunako Old Trafford.

Katika mechi 2 za mwisho alizocheza, Lingard amefunga magoli 2 pekee. Goli la kwanza akilifunga katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Uingereza – EPL dhidi ya Leicester City likiwa ndio goli lake la kwanza la Ligi Kuu tangu mwaka 2018. Goli lake la pili ni dhidi ya LASK katika Michuano ya Europa.

Solskjaer bado anasadikika kuwa shabiki wa Lingard kwani aliwahi kumfundisha wakati akiwa timu ya vijana na hata alipokabidhiwa mikoba ya Mourinho kama kocha mkuu wa kikosi cha Manchester United.

Kushuka kwa kiwango na kuwa na mlolongo wa majeruhi kunatajwa kama vichocheo vya Lingard kukosa namba katika kikosi cha Manchester United. Akiwa na umri wa miaka 27 sasa, ni dhahiri Lingard anahitaji kuonesha uwezo wake na kama ataondoka Man United, basi itakuwa ni fursa kwake kufanikisha hilo.

Lingard na Sanchez ni kati ya wachezaji ambao walionekana kama wameshaoneshwa milango ya kutokea kwa kukosa namba katika kikosi cha kwanza na kukumbwa na majeruhi ya mara kwa mara na hivyo kuwa na muda mfupi sana wa kuitumikia timu.

Sanchez amekatisha mkataba wake wa miaka 2  na Manchester United na kujiunga na Inter Millan ambayo alisajiliwa kwa mkopo. Sasa atasalia huko [Inter Millan] kwa mkataba wa miaka mitatu huku United wakimlipa pauni milioni 7.5, na kuokoa pauni milioni 40 ambazo angelipwa kama mshahara wake kwa muda wote uliosalia katika mkataba wake.


Tiketi yako ya kwanza kamwe haiwezi kupoteza ukiwa na Meridianbet. Unarudishiwa 100% ya Tiketi yako ya kwanza.

Ingia Mchezoni

39 Komentara

    Wanataka Kumuuza Lingard

    Jibu

    Ni muda kwa Jesse Lingard kuondoka Man U#meridianbettz

    Jibu

    popote kambi lingard

    Jibu

    popote kambi lingard kila la kheri uendapo

    Jibu

    Maisha popote Jesse..

    Jibu

    Asante kwa makala

    Jibu

    Mbona mnayumba Man U mtaka kumuuza Lingard kwann jamani

    Jibu

    Aende anapotaka

    Jibu

    Ila sio mbaya maisha popote.

    Jibu

    Mmh Ni sahihi maan wao ndo wanajua uzur wake na ubay wake kwaiyo maamuzi wanayo wao

    Jibu

    Sidhani kama ataondoka lingaad ole ana imani nae

    Jibu

    Popote kaz

    Jibu

    Dah sidhani kama hataondoka lingard

    Jibu

    Kapambane maisha popote

    Jibu

    Akapambane mbele

    Jibu

    Muda wa kuondoka sasa lingard ili mwingine akae kwenye nafasi yako

    Jibu

    Duh man u wanamuuza Lingard!

    Jibu

    Aende tuu akaangalie maisha mengine!!

    Jibu

    Itabid akaangalie timu nyingne abadilishe hal ya hewa maana mpk alikuwa anafanana na timu

    Jibu

    Lingard bora aende tuu

    Jibu

    Maisha popote kijanaa

    Jibu

    Usikate tamaa maisha popote

    Jibu

    Maisha popote hakuna kurudi nyuma.

    Jibu

    Habari njema kwa makocha.

    Jibu

    Lingard ni mchezaji mzuri lakini hivi karibuni hakuwa kwenye fomu endapo kama Man U wataamuuza basi ataongeza hasira na juhudi kwenye timu atakayoenda, Nadhani atarudi kwenye fomu

    Jibu

    Ni mda wa kusepa sasa lingard kaangalie maisha kwingine

    Jibu

    Maisha Ni popote aende akapambane
    #meridianbettz

    Jibu

    Maisha kokote nenda tu#meridianbettz

    Jibu

    Habari njema kwa makocha

    Jibu

    Kikubwa uwezo anao

    Jibu

    Lingard hana haja kubaki man Chester ni vizuri kuchezea vilabu vingi ili habadirishe mbinu za makocha wengine

    Jibu

    Jesse nenda popote utakapoona kuwa pana manufaa na wewe

    Jibu

    lingard alishuka kiwango pale united aende tu kwingine

    Jibu

    Kiwango chake kinalud sasa

    Jibu

    Wenye pesa wajitokeze hasa Kama wake wenye za pale London

    Jibu

    Popote kambi

    Jibu

    Wangempa nafasi mana anaonekana kwamba ndio uwezo wake unaaza vizuri sasa ila uwamuzi ni wao zaidi

    Jibu

    Maisha popote

    Jibu

    Lingard nae amepoa sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.