Mancini: Italia ina Wachezaji kama Bellingham

Kocha wa timu ya taifa ya Italia Roberto Mancini amesema kua nchi ya Italia ina wachezaji wazuri wenye uwezo kama kiungo wa kimataifa Uingereza Jude Bellingham.

Kocha Mancini anasema kua Italia ina wachezaji wanne mpaka watano ambao wana kiwango sawa na kiungo wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Borussia Dortmund Jude Bellingham, Kocha huyo anasema makocha kwenye ligi hiyo wanapaswa kua na ujasiri wa kuwapa nafasi wachezaji hao nchini humo.manciniTimu ya taifa ya Italia ilishindwa kufuzu michuano ya kombe la dunia nchini Qatar ikiwa ni mara pili mfululizo kushindwa kufuzu michuano hiyo, Italia itapata nafasi ya kutetea taji la michuano ya Euro ambayo walishinda mwaka 2021 katika michuano ya Euro ambayo inatarajiwa kupigwa mwaka 2024.

Mancini ana kazi kubwa ya kufanya kwanza ni kuhakikisha timu ya taifa ya Italia inaweza kufuzu michuano ya Euro mwaka 2024 ili kuweza kutetea taji hilo. Italia itakipiga na Uingereza mwezi Manchi kwenye mechi ya kufuzu michuano ya Euro mwaka 2024.manciniRoberto Mancini ameendelea kutilia mkazo kua Italia ina vipaji ambavyo vinahitaji kupata nafasi ili waweze kuimarika zaidi, Kocha huyo anasema nchi kama Hispania, Uholanzi,Ujerumani, na Uingereza wamekua wakiwapa nafasi vijana wao na ndio sababu wamekua wakifanya vizuri jambo ambalo ni tofauti na Italia.

Acha ujumbe