Kocha mpya wa timu ya taifa ya Ureno Roberto Martinez amesema bado nyota na nahodha wa timu hiyo Cristiano Ronaldo bado ana nafasi ya kuendelea kuitumikia timu hiyo.
Kocha Martinez ambaye ametangazwa kua kocha wa timu ya taifa ya Ureno akichukua nafasi ya Fernando Santos ameweka wazi kua nyota Ronaldo bado anabakia kua mchezaji muhimu kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ureno.
Baada ya kocha huyo kutangazwa kua kocha wa timu ya taifa ya Ureno iliibuku minong’ono juu ya nafasi ya Cristiano Ronaldo kwenye kikosi cha timu hiyo, Lakini mwalimu huyo ameonesha bado ana uhitaji na huduma ya nyota huyo kwenye kikosi cha Ureno.
Kocha Martinez amesema Cristiano amekua kwenye timu ya taifa ya Ureno kwa miaka 19 hivo anahitaji heshima kubwa. Kocha huyo amepanga kufanya kikao na mzungumzo na kila mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno na Ronaldo akiwa miongoni mwao.
Baada ya kutolewa kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar kwenye hatua ya robo fainali, Wengi walifikiri kua Ronaldo angetangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Ureno lakini nyota huyo mpaka sasa ameonesha bado anahitaji kuwepo kwenye timu hiyo.