Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayeichezea klabu ya Paris Saint Germain Mauro Icardi amekamilisha uhamisho wake wa kwenda nchini Uturuki kwenye klabu ya Galatasaray kwa uhamisho wa mkopo wa muda mrefu.

Mauro Icardi amekuwa hana furaha tokea alivyoondoka kwenye klabu ya Inter Milan na kuhamia klabu ya PSG ambapo alidhani atapata nafasi ya kucheza mara kwa mara lakini nako amekosa nafasi ya kucheza mara kwa mara pia.

Mauro Icardi, Mauro Icardi Asajiriwa na Galatasaray, Meridianbet

Mauro Icardi atasafiri kwenda jijjini Istanbul leo pamoja na wakara wake, huku karatasi zote klabu ya PSG ikiwa imeshakamilsha huku asilimia kubwa ya mshahara wake utakuwa ukilipwa na klabu ya PSG.

Klabu ya Galatasaray inatumia muda huu ambao dirisha la usajiri nchini Uturuki likiwa limebakisha wiki moja kabla ya kufungwa ili kuimarisha kikosi chao, hadi sasa klabu hiyo imefanikisha kuwasajiri Dries Mertens na Lucas Torreira.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa