Simba dhidi ya KMC vijana wa Manispaa ya Kinondoni kurindima Uwanja wa Benjamin Mkapa usiku wa leo ambapo Simba watakua wenyeji wa mchezo huo.

Klabu ya Simba ambayo inaenda kucheza huo kwa mara ya kwanza msimu huu wakiwa hawana kocha mkuu baada ya timu hiyo kuachana na kocha wake Zoran Maki alietimkia nchini Misri na timu hiyo itakua chini ya kaimu kocha mkuu Suleimani Matola.

simbaSimba ambao ndo wenyeji wa mchezo wanaenda kucheza mchezo huo huku wakiwa wameshinda michezo yao miwili ya awali wakijikusanyia alama sita huku KMC wao wakiwa na alama moja wakifungwa mchezo mmoja na kupata sare mchezo mmoja.

KMC wanakwenda kucheza mchezo huu huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza michezo nane ya mwisho waliyokutana na Mnyama Simba huku ikiwa ni rekodi mbaya kabisa kwa upande wao hivo mchezo huo unatarajiwa kua mkali kwakua KMC wanataka kufuta uteja wao huku Simba wao wakitaka kuendelea walipoishia michezo miwili iliyopita na kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa