Mhamasishaji wa mtandao wa YouTube, Logan Paul amesema kuwa anatarajia kumpeleka bondia Floyd Mayweather Jela kwa kushindwa kukamilisha malipo yake.
Staa huyu wa mtandao wa YouTube anadai kuwa mpaka sasa hajalipwa ada zake zote, na anachoka kusubiri.
“Hapana, hajanilipa malipo yangu yote, kwa sababu anapungukiwa na milioni kadhaa. Hili tunalipeleka mahakamani. Tutaonana mahakamani. Hongera kwa kwenda jela, Floyd.” – Logan Paul akinukuliwa na chapisho la The Mirror.
Staa huyu anasema kuwa awali, aliahidiwa kuwa angelipwa kwa cheque mapema sana, lakini kwa sasa anaona kuwa hahitaji kuwa mvumilibu juu ya hili.

Logan Paul anahisi kuwa Floyd Mayweather anamdharau kwa kuwa yeye ni chipikizi kwenye biashara ya ndondi. Logan Paul amekuwa akifanya utani wa kusisitiza kuwa bondia huyo hana pesa kama anavyotajwa kuwa nazo na kupewa jina la “The Money”
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.


