Chelsea: Mkataba Wa Willian Bado Hapaeleweki

Bado hali ni tete kwa winga Willian kufikia makubaliano ya kuendelea kusalia katika kikosi cha Frank Lampard. Suala la mkataba mpya wa Willian bado ni tatizo katika kufanikisha zoezi hili.

Taarifa mbalimbali zinasema Willian anahitaji mkataba wa miaka mitatu ili asalie Chelsea vinginevyo itakuwa ngumu kwake kusalia. Chelsea wamempatia ofa ya mkataba wa miaka miwili pekee na hivyo utofauti wa mwaka mmoja ndio changamoto.

Willian ambaye ameweka wazi adhima yake ya kuendelea kubaki jijini England, bado hajaweka wazi kama atakubaliana na mkataba aliopewa na Chelsea au ataamua kujiunga na timu zingine zilizopo England.

Totenham na Arsenal ni vilabu vilivyopo England na vyote vinahusishwa na kuitaka saini ya Willian ambaye amekuwa na wakati mzuri katika kikosi cha Chelsea kwa takribani miaka 7 sasa.

Wakala wa Willian – Kia Joorabchian amenukuliwa akisema ” Sidhani kama [Willian] amebadilika kwa namna yeyote. Amekuwa mtulivu muda wote. Tulipokua ofa kubwa kutoka Marekani – MLS ambayo ilimtaka ajiunge nao Julai Mosi – lakini amekuwa akihitaji kumaliza msimu na Chelsea na kisha atafanya maamuzi siku moja baada ya mchezo wao wa mwisho”

“Ana ofa mbili kubwa kutoka Ligi Kuu Uingereza – EPL, MLS na mbili za Ulaya . Ataamua baada ya mchezo wa mwisho”

Chelsea wanaonekana kutosumbuka katika hili kwani wamefanya mabadiliko katika sera yao ya mikataba kwa wachezaji wenye umri wa zaidi ya miaka 30. Mwanzoni walikuwa wanaongeza mwaka mmoja na sasa wanaongeza miaka miwili, hawaonekani wakijiongeza zaidi kufikia miaka mitatu kwa wachezaji wenye umri huo – [Willian anamiaka 31].

Lampard alinukuliwa akisema ” naelewa hali ilivyo kwa upande wa klabu. Nina mahusiano mazuri na Willian lakini sijui maamuzi ni yapi. Kama yatatokea wiki ijayo muda wowote kama anavyosema [Willian], basi ni sawa kwa upande wangu vyovyote vile.”

“Nina furaha sana na Willian, amekuwa na mchango mkubwa kwangu na timu kwa ujumla. Utendaji kazi wake na morali kwenye timu ni kitu kikubwa kwangu na timu kwa msimu huu”

“Ni maamuzi yake na nina yaheshimu. Kama akiamua kuondoka , basi Chelsea pia itapaswa kuendelea kutafuta mshambuliaji mwingine”

Chelsea wameshasajili washambuliaji wawili ambao wanaweza kucheza katika nafasi ya Willian. Tayari wamemsajili Timo Werner na Hakim Ziyech, sasa hivi wanapambana kuitafuta saini ya kinda Kai Havertz.

Chelsea watakutana na Bayern Munich katika mechi yao ya marudiano kwenye Michuano ya Ulaya – UEFA wiki hii. Katika mchezo wa kwanza, Bayern alishinda 3-0. Bado Lampard anawakati mgumu hasa wakati huu ambao Pulisic, Azpilicueta, Pedro na Billy Gilmour ni majeruhi. Wakati Jorginho na Marcos Alonso wanatumikia adhabu.


Tiketi yako ya kwanza kamwe haiwezi kupoteza ukiwa na Meridianbet. Unarudishiwa 100% ya Tiketi yako ya kwanza.

Ingia mchezoni

37 Komentara

    Chelsea inabidi wamuongezee mkataba willian mbona ni mchezaji mzuri tu

    Jibu

    Wamuongezee tuu mkataba William mbona kiungo mzuri sana

    Jibu

    Willian yupo vizuri, aongezewe mkataba

    Jibu

    Willian ni mchezaji mzuri sana hila kwa umri wake hakuna timu ambayo itampa mkataba wa mda mrefu kama yeye anavyotaka.

    Jibu

    Jamani wamwongezee tu mkataba

    Jibu

    Wamwache asepe tu maana Arsenal Wana mtaka na yeye anataka kwenda huko

    Jibu

    wamuongezee tu

    Jibu

    Jamani wamuongeze mkataba.

    Jibu

    William Ni mahili Sana Chelsea wafanye mpango wamwongezee mkataba aendelee kuitumikia vizuri timu

    Jibu

    Kutokana na uchezaji wake William ni bora Chelsea wamsajili tu hiyo miaka anayo itaka ya miaka mitatu tumeona juhudi anazo zifanya haswa kwenye kipindi hichi kigimu cha kuelekea ubigwa kulikiwa na wachezaji ambao wanauwezo kwa sababu ya majeraha waliyo yapata hawakuwa uwanjani ila yeye alijitahidi sana kama inawezekana wamuongezee tu Mimi kama shabiki wa Chelsea namkubali sana.#meridianbettz

    Jibu

    William ni mchezaji mzuri sana kama nafasi ipo msajilini ili aendelee kukipiga chelsea

    Jibu

    Sioni sababu ya blues kumpuuzia William waendelee kuwa nae

    Jibu

    William bado kijana mdogo na nivema akasimamia msimamo wake

    Jibu

    Goodupdate#meridianbet

    Jibu

    bdo mchezaji bora sana apambne zaid

    Jibu

    William kijana mdogo sana na anajua sana

    Jibu

    Chelsea wasipoangalia watamkosa huyo mchezaji

    Jibu

    Willian bado mchezaji mzuri nadhani anaweza pata timu nzuri zaidi ya Chelsea

    Jibu

    Wiliam angeenda Arsenal tu.

    Jibu

    Chelsea waspokaza watampoteza

    Jibu

    Hapa wakala lazma awe mkwel maana siku zote wakala ndo anayetafuta dili ndie mtu wa kwanza kujua mchezaji anaenda wap?

    Jibu

    Mchezaji mzuri

    Jibu

    Muongezeen buana

    Jibu

    Tatizo la willian na Chelsea ni swala la mkataba na soka la sasa huwezi kumpa mchezaji mkataba wa mda mrefu wakati umri wake nao hauruhusu.

    Jibu

    Willium hana maamuzi yake binafsi mwenyewe hivyo akae na timu yake wamalizane

    Jibu

    Bado natumai bado ataendelea kubak Chelsea

    Jibu

    Mchezaji mzuri

    Jibu

    Mchezaji mahiri

    Jibu

    Wamuongezee mkataba tu

    Jibu

    Mchezaji mzuri

    Jibu

    Kiungo bora Sana

    Jibu

    Willian inabidi awe na msimamo

    Jibu

    Wamuongezee tu mkataba jaman

    Jibu

    Mwenzao Anataka kubaki wao hawataki#Meridianbettz

    Jibu

    Waache ubabaifu wamuongeze tu mkataba#meridianbettz

    Jibu

    Naamini Willian atakubaliana na sera ya klabu na kuongeza miaka miwili ambayo klabu ipo tayari kumupa#meridianbettz

    Jibu

    Willian ni kiungo bora mwenye nafasi ya kucheza kwenye timu yoyote hivyo itakua bora zaid kwa Chelsea wakimuongezea mkataba

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.