Nafasi za FIFA

Kukiwa na zaidi ya michezo 150 iliyochezwa mwishoni mwa wiki mbili zilizopita ambayo ilikuwa ikihusisha michezo ya kirafiki na mingine ya kufuzu kuelekea michuano ya Euro 2020; shirikisho la dunia linalojihusisha na mpira wa miguu limeweka wazi nafasi mbalimbali za mataifa ambayo ni wanachama wa shirikisho hilo.

Pamoja na nafasi hizo kupangwa lakini nafasi tatu za juu bado hazijabadilika na zimesalia kama zilivyo pamoja na nafasi nyingine kubadilika kwa waliokuwa chini kupanda juu na waliokuwa juu kushuka chini. Pamoja na mechi za hivi karibuni wengineo wameendelea kujizolea alama za kusalia juu.

Ubelgiji wanaendelea kushika nafasi ya juu kabisa kwenye takwimu hizo za dunia wakiwa wamejizolea ubora wa kukaa hapo baada ya kuonesha kiwango cha pekee kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018 na bado ubora huo unaendelea kuthibitishwa mbele yao kwa kucheza soka la heshima.

Washindi wa kombe la dunia, Ufaransa wanaendelea kushika nafasi ile ile ya pili wakiwa na kikombe cha kombe la dunia mikononi mwao baada ya ushindi na uwezo waliouonesha kwenye michuano hiyo. Pia, uwepo wa kikosi chenye kizazi ambacho kinaonesha uhalisia wa soka lenyewe na kuzaliwa kwa soka upya ndani ya taifa hilo.

Kizazi cha wenye historia ndefu kwenye soka, Brazili kwa kipindi kirefu wamekuwa wakisumbua kwenye hatua za juu za viwango hivyo vya FIFA. Haina ubishi ni taifa ambalo kizazi chake hupotea na kurudi ndani ya kipindi kifupi kutokana na kuwa na wachezaji ambao wana vipaji vya pekee vinavyosumbua ligi mbalimbali walimo wachezaji wake.

Uingereza amepanda nafasi moja juu katika viwango hivyo na kupelekea kumshusha aliyekuwa kwenye nafasi hiyo ambaye ni Croatia aliyekuwa nafasi ya pili kwenye kombe la dunia lakini kwenye viwango hivi anaendelea kushuka kuelekea nafasi za chini kabisa jambo ambalo anaweza kujikuta anapotea kwenye nafasi hizo za juu hadi nafasi ya tano.

Uruguay wamepanda nafasi moja juu kwenye viwango hivyo vya kimataifa baada ya kukaa kwa kipindi kirefu nafasi za chini. Pia, nafasi hizo zimeshuhudia Ujerumani aliyekuwa ameporomoka hadi nafasi ya 13 kupanda kwa nafasi tatu juu kitu ambacho kinaonekana cha pekee sana mbele ya mabingwa hao wa siku za nyuma.

Wengine ni Israel ambao wamepanda kwa nafasi nane juu akifurahia kupanda nafasi hiyo ya juu kati ya mataifa yote, Guatemala amepanda kwa nafasi sita juu, Tanzania nao hawakuwa mbali kwenye kampeni hiyo baada ya kupanda kwa nafasi sita juu ikiwa ni baada ya kushinda mechi yake iliyomuwezesha kukata tiketi ya kushiriki fainali za mataifa ya Afrika mapema mwezi uliopita. Jambo hilo limempa nafasi ya kupanda kwenye nafasi yake.

2 Komentara

    Habar njema

    Jibu

    Habari nzuri

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.