Watford wametengeneza historia upya baada ya kipindi kirefu cha kutokufika hatua hiyo ya fainali. Wamewatupa nje ya michuano hiyo wababe wa Manchester United baada ya kucheza mechi iliyokuwa ya kipekee baina ya wawili hao iliyopelekea kuchezwa kwa zaidi ya dakika 90 za mchezo za kawaida.
Ni kipindi kirefu tangu Watford wafikie hatua hiyo ya fainali kwenye kombe la FA lakini kwa sasa wameweza kufikia hatua hiyo upya tena. Waliwahi kufikia hatua hiyo mwaka 1984 na sasa wameweza kufanya hivyo. Kwao kufika hapo ni historia mpya kwenye michuano hiyo na ni hatua kubwa sana kwa msimu huu.
Alikuwa ni Deeney aliyewarejesha mchezoni dakika ya 94 ya mchezo baada ya kupata mpira wa adhabu ambayo iliwafanya wasawazishe makosa kutoka kuongozwa 2-1 na kwa dakika hiyo kufanya matokeo kuwa sare jambo lililopelekea mechi kusonga mbele kwa dakika 120 zaidi ili kuamua nani asogee kwenye fainali.

Kitu ambacho ni kikubwa katika mechi hiyo na kimekaa kama cha kihistoria ni pale alipoingia Gerald Deulofeu na kufanya maajabu ndani ya kipindi kifupi na kuweza kuibuka kama mchezaji aliyekuwa amebeba bahati nzima ya kuwapeleka Watford mbele kwenye michuano hiyo. Nyota huyo alizama nyavuni mara mbili na kuwafanya Watford kuondoka na furaha kubwa.
Hii inaonesha kwamba Watford wameweza kufikia hatua hiyo kwa sasa baada ya mwaka 1984 walipopoteza mbele ya Everton na kumfanya mmiliki wao wa kipindi hicho kutoa machozi baada ya timu yake hiyo kupoteza. Mmiliki wa kipindi hicho alikuwa mwimbaji Elton John ambaye kwa sasa ni Rais wa klabu hiyo wa maisha.
Mwimbaji huyo kwa sasa ana filamu aliyoipa jina la Rocketman ambayo ataiachia mapema mwezi Mei siku kadhaa baada ya klabu yake kuvaana na Manchester City kwenye fainali za kombe hilo. Na mechi hiyo itafanyika pale Wembley ikiwa ni katika hatua ya kutafuta bingwa wa michuano hiyo atakayeondoka na kikombe hicho.
Fainali hiyo itakuwa ya kwanza kwa kikosi hicho cha Javia Gracia; Mhispania huyo anastahili pongezi na sifa nyingi kwa makubwa aliyoyafanya na kikosi hicho cha Watford na historia aliyoifikia. Hilo ni kutokana na kupigana kutoka kufungwa magoli mawili hadi kuweza kuondoka na ushindi kwenye mechi hiyo.
Mara zote kwenye hatua hiyo lazima mmoja aumie ili mwingine aweze kufurahia na hilo lilionekana hata kwenye mechi hiyo baada ya furaha iliyooneshwa na upande huo wa Watford kwa namna walivyoweza kushangilia ushindi huo kwamba ilikuwa ni kiu yao ya muda mrefu kushinda taji au angalau kufika fainali za kombe hilo; jambo ambalo kwa hakika wamefanikiwa kulifikia.


Povel tz
Gud news