Philipe Countinho Hana Mpango na EPL Tena

Staa wa Barcelona Philipe Countinho anasisitiza kuwa na furaha klabuni Barcelona, na kuwa hana mpango tena na Ligi Kuu ya Uingereza. Philipe alikuwa anahusishwa kusepa Barca wakati akikanusha kurejea tena EPL.

Staa huyu alisepea Barcelona akitokea Liverpool Januari 2018 kwa ada inayotajwa kuwa paundi milioni 160, akiwa klabuni hapo alifanya bidii sana ili aweze kupata namba ya kudumu klabuni hapo.

Klabu za Manchester United na Chelsea ndiyo zilikuwa zinahusishwa zaidi na staa huyu, bahati mbaya kwao Countinho hana mzuka na EPL na hatarajii kurudi huko siku za usoni.

Philipe Countinho Hana Mpango na EPL Tena

Countinho akizungumza na The Mirror wakijiandaa kukutana na Man United kwenye robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya United, ansema;

“Kichwa changu kinafikilia kuhusu Barcelona tu. Kurejea Uingereza hakuna nafasi kwenye mipango yangu. Huu ni msimu wangu wa pili, na nimeshindsa mataji. Mimi ni mchezaji ambaye nina ndoto kubwa na nahitaji mataji zaidi. Ninafuraha, nilitamani kucheza Hispania na nipo kwenye klabu bora hispania”

 

 

6 Komentara

    Habari njema

    Jibu

    Coutinyo binge la mchezaji anajiamini akiwa uwanjani ingawa hataki kuja Uingereza Ila nafkiri bado ananafasi pale na ndipo alipowika akiwa EPL

    Jibu

    Coutinyo bonge la mchezaji anajiamini akiwa uwanjani ingawa hataki kuja Uingereza Ila nafkiri bado ananafasi pale na ndipo alipowika akiwa EPL

    Jibu

    Countinh nimchezaji mzuri Sana hanejua kibaji chake nakujielewa nn anafanya na pia akiwa uwanjani ujiamini pia Kama yupo kwenye kaz yake yakupamba kwaio namkubali Sana napia mchezaji ane jielewa

    Jibu

    Bora arudi tu mana kafichwa sana

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe