Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea raia wa kimataifa wa Ufaransa Christopher Nkunku amepata majeraha tena ambayo inaelezwa yanaweza kumuweka nje ya uwanja kwa wiki tatu mpaka nne.
Ikumbukwe Nkunku hana muda mrefu tangu atoke kwenye majeraha ambayo yamekua yakimsumbua mara kwa mara, Huku taarifa zikitoka kua mchezaji huyo amepata majeraha tena ambayo yatamueka nje tena kwa wiki kadhaa.Mshambuliaji huyo amekua akisumbuliwa na majeraha ya goti tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea klabu ya Rb Leipzig, Jambo ambalo limekua likiitesa klabu hiyo kwani ni moja ya wachezaji waliotarajiwa kufanya makubwa ndani ya timu hiyo.
Kutokana na majeraha aliyoyapata mchezaji huyo ni wazi mchezaji huyo hajafanikiwa kukaa hata miezi miwili akiwa fiti ndani ya timu hiyo tangu ajiunge, Kwani majeraha yamekua na yeye kwa muda mwingi tangu ajiunge na klabu hiyo.Mshambuliaji Nkunku hali hii inamuumiza pia yeye kama mchezaji kwani alitarajia kufanya makubwa ndani ya timu hiyo, Lakini kinachotokea ni tofauti kwani majeraha yamekua hayamuachii afanye ambacho ana uwezo mkubwa wa kukifanya.