Kiungo wa klabu ya soka ya Arsenal Martin Odegaard amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Novemba na Disemba wa ligi kuu ya soka ya Uingereza.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Norway amekua na kiwango bora sana ndani ya klabu ya Arsenal ambao ni vinara wa ligi kuu ya Uingereza. Odergaard amekua moja ya wachezaji muhimu zaidi ndani ya kikosi cha Arsenal chini ya kocha Mikel Arteta.odegaardMartin Odergard amefanikiwa kucheza michezo minne ndani ya mwezi Novemba na Disemba na kuweza kuhusika kwenye mabao sita katika michezo hiyo. Kiungo huyo amefanikiwa kufunga mabao matatu na kutengeneza mengine matatu huku akihakikisha klabu yake inashinda michezo yote minne.

Klabu ya Arsenal ipo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza kutokana ubora mkubwa ambao amekua wakiuonesha ndani ya msimu huu, Lakini pia nahodha wao ambaye ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi akiwa moja ya mihimili muhimu zaidi klabuni hapo.odegaardMartin Odegaard ambaye alitoka klabu ya Real Madrid kwa mkopo huku sasa akiwa ni mchezaji rasmi ndani ya klabu hiyo, Amefanikiwa kuonesha kiwango cha juu klabuni hapo msimu huu na hiyo ni baada ya kupata nafasi mbele Eddie Smith Rowe aliepata majeruhi na kumfanya kiungo huyo kupata nafasi ya kudumu kikosini.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa