Nyota wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo ataukosa mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Crystal Palace msimu huu kutokana na majeruhi ya “hip flexor”

Majeraha haya yamekuwa yakijirudia rudia kwa Ronaldo, pia yamemuweka nje ya uwanja mara kadhaa na kukosa baadhi ya michezo msimu huu. Mchezaji mwingine ambaye atakosa mchezo wa leo ni Paul Pogba ambaye anahusishwa na kuhama klabu hiyo baada ya mkataba wake kuisha msimu huu.

Ronaldo

Kocha mpya wa klabu ya Manchester United Erik ten Hag anatarajiwa kuwepo kwenye dimba la Selhurst Park ili kuweza kuangalia kikosi chake ambacho anataka kufanya nacho kazi huku akiahidi kifanyia  mabadiliko makubwa.

Ronaldo amekuwa kwenye kiwango mzuri msimu japo kuwa klabu ya Man United haikuwa na msimu bora na amefanikiwa kufunga magoli 24 kwenye michezo 39 aliyocheza katika mashindano yote msimu huu.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno kwa sasa anajiandaa kwenye msimu mpya wa mashindano ya UEFA Nations League, ambayo yanatarajia kuanza mwezi June, huku wakianza kampeni hiyo dhidi ya Hispania na siku tatu baadae watacheza na Switzerland.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa