Nyota wa Juventus Cristiano Ronaldo anasema kuwa amefanikiwa kwa asilimia kubwa malengo yake akiwa klabuni Juventus.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ronaldo ameandika ujumbe mzito juu ya safari yake ya soka akiwa na Juventus na mafanikio aliyoyapata.
Ronaldo ameainisha kuwa sehemu ya msingi ya kupima mafanikio, ni kuanza kutazama kuanzia mtu binafsi mpaka na kisha mchango wa kila mmoja anayehusika na klabu katika kufanikisha jambo kama timu.
Licha ya kushindwa kutetea taji la Serie A msimu huu, Ronaldo amewapongeza Inter kwa jitihada zao na kustahili kutwaa taji hilo. Kwake ni muhimu kutambua mchango wa kila mmoja na timu kwa ujumla.
Akitaja Italian Super Cup, Italian Cup na kuwa mfungaji bora Serie A kwake ni heshima kubwa hasa kwa nchi kama Italia ambayo ni vigumu kushinda kitu chochote.
“Kwa mafaniko haya, nimefikisha lengo ambalo nilijiwekea mimi binafsi tangia siku ya kwanza nilipofika Italia. Kushinda Championship, Kombe na Super Cup na kuwa mchezaji bora na mfungaji bora kwenye nchi kubwa kisoka yenye wachezaji mashuhuri, vilabu vikubwa na utamaduni wa kipekee wa soka”
Je Ronaldo anaondoka Juventus?
Ujumbe wa staa huyu umezua sintofahamu, japokuwa hatma ya staa huyu bado haijawa wazi. Awali ilibainishwa kuwa mpango wake ulikuwa kuondoka Juventus ikiwa wangeshindwa kufuzu kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lakini Juventus wamefanikiwa kufuzu dakika za mwisho, lakini bado Ronaldo anahusishwa na kuondoka klabuni hapo, licha ya kuendelea kuwa na ukungu kwenye suala lake.
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
Pongezi kwake