Sadio Mane ni nyota msenegali anayekipiga klabuni Liverpool. Amekuwa na historia ya kipekee katika soka na aliamua kutengeneza picha ya hisitoria ya maisha yake hadi alipofanikiwa kucheza soka la kulipwa.

Katika picha ya maisha yake, “Made in Senegal” Sane amejaribu kuuambia ulimwengu kuwa kila safari ya mafanikio huwa siyo rahisi. Alipitia changamoto kadhaa kufika alipofika, kuna baadhi ya mambio katika safari yake yanafurahisha na mengine yanatia majonzi lakini ni fursa ya kujifunza kila uchwao.
Baadhi ya mambo ambayo unaweza kuwa umeyasikia, ila haukuwa na uhakika kuhusu staa huyu, hapa baadhi ya vitu vilivyovutia wengi kuhusu maisha ya staa huyu ni kuwa aliwahi kutoroka nyumbani!
Staa huyu alilelewa zaidi na wajomba zake, na alisisitizwa zaidi kuwekeza bidii katika masomo. Familiya yake walikuwa wacha mungu na alikulia katika malezi haya ya kumcha mungu ya dini ya kiislamu.

Kama ilivyo ada! Wazazi wanataka watoto wabukue, hiyo huwa ni furaha kwao! Mane alikuwa anapata majanga kila siku kwa sasbabu Mjomba wake alipendelea zaidi asome shule sio kucheza soka na alikuwa anamuwekea mazingira fulani ya kumzuia.
“Mjomba hakutaka nicheze nicheze kwa sababu alifikiri shule ndiyo ilikuwa muhimu zaidi. Mambo yalikuwa magumu kwa sababu hakupenda”
Sadio Mane
Mwaka 2008, akiwa na umri wa miaka 16 Sadio Mane alilazimika kutoroka kijijini kwao Bambali nchini Senegal ili akacheze soka tu! Lakini alikamatwa na kurejeshwa nyumbani. Nyumbani walikubaliana alikubaliana na familia yake kuwa mwaka unaofuata angeruhusiwa kucheza soka kadri apendavyo.
Mane ansema baada ya hapo ilikuwa ni “soka, soka, soka”! Yaaani soka kwa kwenda mbele!


Frank patrick
Mapambano ya waafrika ….wacha awe mchezaji bora na mchaMUNGU aisee
Ally mohamedi ally
Muache awe mchezaji bora kapambana sana
Theckla
Kipaji anacho kikubwa tu …..
Dee
Jamaa yuko vizuri…..
David Pere
Kweli kila Jambo Lina sababu zake Yani kutoroka kwake,kumemfanya kuwa bilionea duniani
Zuhura omary kindamba
Sadio mane ni mchezaji mzuri sana
Aziza mushi
Yupo vizuri na ana kipaji Sanaa
mwakalosi
Afrika tunapambana sana hasa magharibi wanapambana sana huku mashariki tuko na uvivu uvivu
Flomena
Kipaji toka kwa mungu
Leonard
Mafanikio sio rahisi kama tunavyodhani
Omary lukumbi
Mafanikio siku zote hayako njia moja tuu maana hata mungu anaweza kukunyanyua kwa njia nyingine tofauti tunayo fikilia sisi binadam na ndio falsafa za watu wa Africa tunaamini shule pekee ndio inaweza kumkwamua mtu kwenye dimbwi la umaskin tunasahau kua mungu kua kila mwanadamu amempa njia zake za ridhik
Hamidu
Mane mchezaji mwenye kipaji .. anafanya makubwa Sana pale Liverpool#meridianbettz
Samira
Na amedhihilisha kwamba yeye kipaji cha mpira anacho maana ni mchezaji anaejituma sana
Adelta
Amezaliwa na kipaji chake
Fatuma kasomo
Jamaa kipaji anacho
Dorophina
Mane yupo vizuri huenda asingetoroka tusingemjua alipambania kipaji chake mpaka kufanikiwa
caroline
kweli tujifunze kutambua vipaji vya watoto
mwajuma
Anakipaji kizuri sana jamaa
Magdalena
Jamaa yupo Bomba na anatambua nini anafanya
Genia Sikaluzwe
Jamaa ni fundi mpira na piya huwa anatambua ancho kifanya uwajani
isha
Mane nimeikubali hisitolia yako uko vizuri sana na pia ulijitahidi kupambana
Mwanahamisi
Jamaa Yuko vizuri
Tatu
Waafrica sasahv tunajitahi sana tofauti na kipindi cha nyuma wazungu walitubuluza sana kwenye soka
Zeiyana
Asante kwa taarifa hii so tulikua hatujui kama mane kipaji chake toka moyoni mane alipambania sana kipaji chake hadi leo hii tunaisoma histor daah..!kweli ukipambania ndoto yako unafanikiwa kwa haina yake big up sadio mane
Lydia Emmanuel Magoti
Jamaha yupo vizuri nakipaji anacho
felister
Sadio mane soka soka ,soka daymuni
Mariam mtandama
Kiukweli yupo vizur sana
Franky
Utoto ulikua una msumbua uyu kijana
Ester jackson
Kweli kabisa mafanikio hayaji kirahisi kabisa mane aliona kipaji chake mapema sana mpaka hasaivi anakuwa mchezaji bora historian yake inasisimua sana na kufundisha kuwa tusikate tamaa na kutokukubali ndoto zetu zisiweze kuzimwa.
Revina
Kipaji alikitambua mapema ndo maana akatoroka na utundu umemsaidia Mane
Ester mmakasa
Masikini kumbe anahistoria jamaa kiukweli anafanya mambo mazuri sana.
Povel tz
Mane mtu mbaya sana kwny soka
Povel tz
MANE tumain jipya litakalochukuwah ballon d’or
Ernest
Hapa nimejifunza kuwa hatutakiwi kukata tamaa, Safi sana Mane the Dream chaser
lombo
riziki ya mtu hupangwa na .mungu
Rehema
Huyo jamaa Yuko vizuri
Njiku
Dah hii ipo poa sanaa
Edgar
Ni maamuzi mazuri coz yamekupa mafanikio makubwa
Amiri Kayera
Safii
Samiah
Kipaji moyoni
Gabriel
Katika wachezaji ninaowakubal manw namkubali sana katika historia yake Mane alipotoka Senegal kwenda Ufaransa alijiunga na timu ya Metz mwaka 2011. Na kitu pekee alicho kipitia na kikampa wakati mgumu kwa mwezi January kule Ufaransa ni baridi. Mane alielezea jinsi wachezaji wenzake walivyo mshangaa baada ya kutoka na Sweta kwenye chumba cha kubadirishia nguo “walianza kucheka na sikujua wanacheka nini “ ikabidi awaulize “waka niambia inakuaje unavaa hivyo?”
Mane anasema kipindi alichokipitia FC Metz ndio kimemfanya kua Mane tunae muona leo, Mwanzoni mwa utumishi wake pale Metz alipatwa na tatizo la nyonga ila hakuwahi kumwambia mtu yeyote kwasababu ya kuhofia kurudishwa Senegal.
Hivyo safar yake ilikuwa yenye kuhamasisha sana
Issa
Mane kipaji
devotha
hongera sana Sadio Mane kwa kuhakikisha ndoto zako zinatimia
Furahav
Habari nzuri
Hope mwaikuka
Yuko vzur
Salma
Ana kipaji kikubwa
Sadick
Senegal ina vipaji vingi sana ukiachilia mbali Saidio Mane. Wazazi wengi wanapenda sana watoto wasome si kucheza mpira#meridianbettz
Shafii
Mane kapambana Sana.
warda
Alifanya poa sana#Meridianbettz
sabrina
Jamaa anajua sana