Simba Kimataifa Hafiki Popote - Zahera

Mwinyi Zahera, Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi ndani ya Klabu ya Gwambina FC amesema kuwa Simba hawatafika mbali kwenye michuano ya kimataifa ikiwa watacheza kama walivyocheza na wao.

Zahera aliwahi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga msimu wa 2018/18 na 2019/20 alipigwa chini kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni timu yake kuboronga michuano ya kimataifa.

Simba, Septemba 26 ilicheza na Gwambina mchezo wa Ligi Kuu Bara na kushinda mabao 3-0 ukiwa ni mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.

Zahera amesema kwa namna ambavyo Simba walicheza hamsini kwa hamsini na kama watacheza hivi kwenye mashindano ya kimataifa hawatafika kokote.

“Nimeona Simba ikicheza ni inacheza vizuri na inapenda kucheza mpira wa pasi, sasa ukiangalia namna ambavyo walicheza na timu yetu ni kwamba tuliweza kwenda nao sambamba mwanzo mwisho licha ya kwamba tumepoteza.
“Wana kazi kubwa ya kufanya kimataifa hasa kwa aina ya mchezo wanaocheza, kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hawatakutana na timu kama hizi za kwetu, kule kuna TP Mazembe wao wanakuja muda wote hawajui habari za pasipasi ni kucheza kwa nguvu mwanzo mwisho.
“Kama mwendo wao utakuwa ni hivi basi itakuwa ngumu kufika mbali kwenye michuano ya kimataifa kule kunahitaji nguvu nyingi na spidi muda wote ili kushinda.” amesema.


Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!

Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!

Soma Zaidi

35 Komentara

    Wanatakiwa wafanye vizuri zaidi ya hapo ili wafike ngazi ya kimataifa.

    Jibu

    🔥

    Jibu

    Simba waongeze bidii

    Jibu

    Zahera yupo sahihi kama ni wasikivu ni swala la kulifanyia kazi

    Jibu

    mh simba wanabidi waongeze juhudi za kutosha ili waweze kufika mbali zaidi

    Jibu

    Bora aongeze bidii

    Jibu

    Simba ni wa kubahatisha tu!!!

    Jibu

    Hamna kitu maneno mdomoni tuu ila mpila haujachezwa mpaka wamefika apo ujue Simba wanajimudu na watakabiliana timu yoyote ile ili kuonyesha ushujaa wao nawakiwa na umoja kilakitu kitaenda sawa nawa kubali Simba

    Jibu

    Watafika tu endapo wakiwa na umoja

    Jibu

    Simba blah blah nyingi.

    Jibu

    Simba kwa sasa wanakikosi kizuri lakini uwanjani amna kitu wasipokuwa makini msimu huu hawatafika mbali

    Jibu

    Simba wakijipanga watafika mbali

    Jibu

    Simba kimataifa inaweza kufika mbali ila ni uwezo tu wa wachezaji kujituma zaid na wasilew na mafanikio ya ligi watakiwa wajijfue na kupata michezo kirafiki ya kimataifa ili wazoee

    Jibu

    Haya tutafanyia kaz ushaur wako

    Jibu

    Ni ushauri mzuri kwa simba sport

    Jibu

    Simba wapo vizuri

    Jibu

    Simba walicho jiaminia wao kusajili mabeki nane ndio wameona washamaliza kazi subiri tuone mwisho wa mchezo ni bora tu ulivyowapa mapema habari zao mwinyi zahera

    Jibu

    wanakikosi kizuri lakini uwanjani amna kitu wasipokuwa makini msimu huu hawatafika mbali

    Jibu

    Maneno tuu hayo na iyo kazi ya utabiri umeipata wapi au ndio njaa za mjini,simba kama simba kelelee nyingi kwa simba akeeeee!!!

    Jibu

    Simba kwer ina team nzur Ila inaitaj Zaid kujiandaa vzr

    Jibu

    Simba michuano ya kimataifa haiwz kufika mbali uwezo wa wachezaj walionao ni wa kufua ndani ya ligi si kimataifa zaidi

    Jibu

    asante meridianbet kwa habar moto moto

    Jibu

    Simba wajipange

    Jibu

    Simba wajipange tena wajipange haswa!

    Jibu

    ushauri mzuri

    Jibu

    Maneno tu ayo

    Jibu

    Simba wanakikosi kizuri tu sema kikubwa ni kuongeza juhudi na nguvu zaid katika kikosi

    Jibu

    Simba ni noma

    Jibu

    Mmh hay maneno yako tu simba chama kubwa

    Jibu

    Huyo zahera hana jipya hayo ni maneno ya mkosaji tuu

    Jibu

    Umoja ni nguvu wana simba inabidi washikamane

    Jibu

    Simbaa ndio baba lao hakuna kama simbaaa

    Jibu

    Asitafute kiki hapa apambane na hali yake

    Jibu

    Ngoja tuone Zahera Yanga huyo majungu majungu tuu

    Jibu

    wanakikosi kizuri lakini uwanjani amna kitu wasipokuwa makini msimu huu hawatafika mbali

    Jibu

Acha ujumbe