Klopp - Tutatetea Ubingwa

Jurgen Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa timu hiyo ina jukumu la kuendelea kushinda kila mechi ndani ya Ligi Kuu England ili kuweza kutetea taji lao.

Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe hilo usiku wa kuamkia leo waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Arsenal inayonolewa na Mikel Arteta kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Anfield.

Arsenal ilianza kuwatungua Liverpool dakika ya 25 kupitia kwa Alexandre Lacazette lilidumu kwa muda wa dakika mbili pekee kwani Liverpool waliweka mzani sawa kupitia kwa Sadio Mane dakika ya 28.

Wakati Arsenal inayomtegemea Pierre Emerick Aubameyang kwenye upande wa kutupia mabao ikihaha kutafuta ushindi ilitunguliwa bao la pili dakika ya 34 na Andrew Robertson na dakika ya 88 msumari wa tatu ulipachikwa na Diogo Jota.

Klopp amesema kuwa ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kushinda tena taji la Ligi Kuu England kazi yao ni moja kuendelea kushinda mechi zao zote.

“Haikuwa rahisi ila nimeona kiwango cha wachezaji ni kizuri wananifurahisha wamefanya vizuri na kazi ni moja tu kutafuta ushindi,” amesema.


Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!

Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!

Soma Zaidi

34 Komentara

    Safi sana

    Jibu

    Liverpool ya msimu huu n moto

    Jibu

    Ligi ndo imeanza tusubirie mzunguko wa kwanza uishe apo ndo tutakuwa na majibu

    Jibu

    naona klopp anataka wachukue tena taji msimu huu ataki kabismasihara

    Jibu

    Hanacho kisema Klopp kipo sahii anataka kuja Tena kivingine kuja kuchukua tena taji ataweza tuu navyo muerewa mzee huyo yupo makini natimu yake

    Jibu

    Kandanda limeanza, tunasubiri kuona nani atachukua ubingwa?

    Jibu

    Kloop anajiamini sana na kwakweli wako vizuri na timu yake.

    Jibu

    Klopp yupo vinzur kwenye timu yake

    Jibu

    Safi Sana Klopp endelea kutengeneza mikakati mtetee taji la ubingwa

    Jibu

    Klopp msimu huu Nina Imani nae kabisa kombe la kwake maan wameanza kwa speed ya 4G

    Jibu

    Klopp yuko vizuri

    Jibu

    Ni ngumu sana kwa kuchukua ubingwa mara 2mfululizo kwa ligi yeny ushindani kama epl

    Jibu

    Nawaaminia sana

    Jibu

    Klopp anajiamini sana

    Jibu

    Klopp yupo sahii ni kweli Liverpool wanakila sababu ya kushinda ligi zote ukiangalia wanakikosi vizuri

    Jibu

    Safi

    Jibu

    tusubirie mzunguko wa kwanza uishe apo ndo tutakuwa na majibu

    Jibu

    Jitihada zinaitajika kutimiza malengo yenu

    Jibu

    Ni mipango mizur Ila ni ngumu

    Jibu

    Kuchukua epl mara 2 mfululizo ni ngumu hasa kwa ligi ya uingereza

    Jibu

    asante meridianbet kwa habar moto moto

    Jibu

    Klopp anamipango ya kutetea ubingwa

    Jibu

    anajitahidi kiasi chake ila ligi ndo kwanza imeanza tusubirie tuone mbele itakavyokua

    Jibu

    Klopp Yuko vizuri kwa Kasi hii lazima achukuwe ubigwa

    Jibu

    Klopp yupo vizuri

    Jibu

    Klopp yupo vizuri

    Jibu

    Klopp yuko vzuri

    Jibu

    Hiyo ndo Liverpool ya mwendo kasi

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Kutetea ubingwa kaz maan kila team inakukamia

    Jibu

    Liverpool wananafasi mkubwa ya kutete ubingwa

    Jibu

    Hanacho kisema Klopp kipo sahii anataka kuja Tena kivingine kuja kuchukua tena taji ataweza tuu navyo muerewa mzee huyo yupo makini natimu yake

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.