MAMA mzazi wa Luis Suarez aitwaye Sandra alikuwa ni mfagizi katika moja ya kituo cha mabasi katika kitongoji cha Tres Cruzes Jiji la Montevideo nchini Uruguay na hakuwahi kukata tamaa kuhusiana na mwanaye kwamba atakuja kuwa mtu mkubwa na maarufu siku moja duniani.
Katika kitabu chake cha Luis Suarez, Crossing The Line, Suarez ameelezea namna Sandra alivyokuwa akihangaika na watoto wengi aliokuwa akiishi nao licha ya umasikini wake na kufanya asiwe na muda wa kumuuliza kuhusiana na shule hasa maendeleo yake.
Pamoja na hivyo, ameeleza namna mama yake alivyoendelea kumpa moyo na kumuasa kuendelea kupambana kwa kile anachokiamini kwa kuwa hakupenda kumpangia. Baba yake mzazi, Rodolfo Suarez alikuwa ni mwanajeshi, baadaye akaamua kuondoka jeshini na maisha yakawa magumu zaidi hadi kufikia kuanza kujitafutia riziki kwa kufanya kazi katika kiwanda cha biskuti na baadaye kuamua kujihusisha na ujenzi. Kuna wakati Rodolfo hakuwa hata na fedha ya kujilipia kodi ya pango tu na kulazimika kulala katika eneo walilokuwa wakifanya ujenzi ili kujisitiri.
Suarez anazungumzia namna umasikini ulivyowafanya wazazi wake washindwe kwenda kumuunga mkono wakati akienda mazoezini katika klabu ya watoto ya Nacional, moja ya klabu maarufu nchini Uruguay. Pamoja na hivyo, Suarez ameeleza anavyoendelea kuwashukuru wazazi wake kwani licha ya kutomuunga mkono kwa vitendo walikuwa wakimpa maneno ambayo yalimfanya aendelee kupambana bila ya kuchoka na mwisho anamtaja mkewe Sofi Balbi kuwa ndiye shujaa wake.
Suarez na Sofi sasa wana watoto watatu, binti Delfina (alizaliwa 2010) na wavulana wawili, Benjamin (alizaliwa 2013) na Lauti, aliyezaliwa 2018. Walianza kuwa wapenzi Suarez akiwa na umri wa miaka 15 na Sofi akiwa na 13.
Mshambuliaji huyo mtukutu sasa ana umri wa miaka 13 na chanzo cha mafanikio yake ya mpira ni Sofi na ndiyo maana anamuona ni shujaa wake lakini mji ulio katika historia ya maisha yake ni Barcelona.
Huenda hapa inakuwa ni nafasi nzuri ya kujua kisa cha yeye kufikia kumwaga chozi wakati anaondoka katika klabu hiyo na kwenda kujiunga na Atletico Madrid ambao ni moja ya wapinzani wakubwa wa Barcelona kutoka katika Jiji la Madrid. Baada ya kocha mpya wa Barcelona, Ronald Koeman kuonekana hana mpango wa kumtumia au hana mpango naye, ikaelezwa atajiunga na Juventus ya Italia na kuungana na Cristiano Ronaldo.
Akiwa katika hatua za mwisho, ikabainika kuwa alifanya udanganyifu wakati akitafuta uraia wa Italia ambao anao. Hivyo ikawa ni kesi ambayo mwisho ilionekana anastahili kubaki nao lakini kukawa na ugumu tena kujiunga na Juve. Ofa ya Atletico, mwisho imefanikiwa kama mchezaji huru lakini mwisho aliangua kilio kama mtoto akijua anaondoka Barcelona.

Wengi wanaweza kudhani ni mapenzi pekee na klabu hiyo ambayo wana kauli mbiu yao “Zaidi ya Klabu”. Suarez lazima atakuwa anakumbuka maisha ya Barcelona ambayo alijiunga nao mwaka 2014 akitokea Liverpool na kufanikiwa kuichezea mechi 191 na kufunga mabao 147, hivyo kuandika rekodi ya kuwa mmoja wa washambulizi hatari zaidi waliowahi kuichezea Barcelona.
Itaendelea..
Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!
Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!



Janeflora malisa
🔥
Antony Luseno
Uenda suarez ndoto zake zilikuwa ni kutumikia barca adi atakapostaafu soka
magdalena
suarez alikuwa anataka kuitumikia barca kama messi lakini ndoto zake zinaonekana hazikutimia
Lydia Emmanuel Magoti
Aki yake Suarez kutoa chozi alikuwa anataka kuitumikia Barcelona mwanzo mwisho kwaio kila chenye mwanzo kina mwisho
Sauda
Suarez ana mapenz na Clab yake ndiyo maana alikuwa hataki kuhamia popote.
Ester mmakasa
Ni historia ya kusikitisha sana na yenye mafunzo kwa wote ni kutokata tamaa ya maisha yako.
Venerose
Alikuwa mzalendo na clab yake
Caroline
Dahh Asante kwa taarifa
Dorophina
Inaonekana wamemkatisha Suarez ndoto yake ya kutaka kuitumikia Barca mpaka mwisho wa maisha yake
Shani
Suarez alikuw na wakat mzur Barcelona na kombineshen yake na mess ilikua mahir kwenye ufungaji
Hopemwaikuka
Usijal hata huko utakua poa tu
Hidaya
Suarez ameshindwa kutimiza ndoto yake
Mwanahamisi
Gud news
Zeiyana
Hayo ndio maisha ya mpira Suarez kila kitu kinaenda na wakati hata sehemu huliyopo ni sahii pia hinaweza ukafanya mkubwa kushindwa hata ya pale na ndio hinavyo kua kila kiongozi anapoingia kwenye madaraka yake lazima hapange yake ili kujenga kitu kiwe kwenye ubora hanao taka yeye yote kwa yote nia yake kukijenga kikosi kiwe kwenye ubora
Fatuma kasomo
Gud news
Gabriel
suarez ndoto zake zilikuwa ni kutumikia barca
Rose kapinga
Barcelona wamekatisha malengo ya suarez
Amiri Kayera
Km mchezaj maisha popot tegemea
Issa
Amefanya makubwa barca na kombineshen yake na mess ilifanya atupie
Magoli sana
lombo
duh hatar
Sabrina
Sio kila ndoto zinatimia hata kama alikua na mpango wa kumalizia mpira barca anatakiwa kuangalia alipo sasa asitazame alipotoka
felister
kiukweli Barcelona wamemkatili Suarez
Adelta
Mashabiki tunashukuru kwa makala nzuri
Saupha mohamed
Suarez anaipenda club yake
Mwajumah
Suarez ameshindwa kutimiza ndoto yake
Nasra
Gud news
Fatina mfigi
Mmmh
Elika
Moyo wa Suarez bado uko barca
Khadija
Good
Asia Abdy
Aaw 😥
aisha
Historia yake inatia motivation
David Pere
Suarez alikuw na wakat mzur Barcelona na kombineshen yake na mess ilikua mahir kwenye ufungaji