Simon Msuva, Muda Haudanganyi

Nipeni biblia nipitie Wathesalonike 4:11-12 nitachukua kalamu yangu na karatasi kudokoa mistari kadhaa “Jitahidini kuishi maisha ya utulivu, kila mtu akishughulikia mambo yake mwenyewe na kufanya kazi kwa mikono yenu”… Tuweke nukta kidogo, Mimi sio mbobezi wa Theolojia.

Wathesalonike inahitaji tuishi kwanza maisha ya utulivu, hapa naitazama sana safari ya Simon Msuva, kuanzia mitaa ya Temeke kwenye dimba la hayati Mkapa, zile kelele za Wananchi juu ya kuihujumu Yanga mbele ya Simba, mpaka kupewa kiroba cha mchele kutoka Mbeya, alichagua utulivu.

Wathesalonike imetuasa sana kuwa kila mtu ashughulikie mambo yake mwenyewe, basi nami namkumbuka sana Simon Msuva aliesafiri zaidi ya masaa 10 angani, akiachana na Mzee Happygod Msuva na Mama yake, mpaka Difaa Hassan El Jadida pale Morocco, ni safari hii ya njia panda Ulaya.

Kwenye kushughulikia mambo yake Msuva hakupitia kurasa ya Mrisho Ngassa aliefika London ya Magharibi pale West Ham United, wala hakupitia ule mstari wake Settle Sounders Marekani, mwisho hakutazama wapi alipo Ngassa Leo hii, yeye akachagua kuishi kwenye Wathesalonike 4:11-12.

Kwenye kushughulikia mambo yake mwenyewe wala hakupitia kurasa ile ya Shaban Iddi Chilunda kutoka Tenerife pale Spain, hakuwaza kuwa kipaji kile kimeshindwa maisha Ulaya, hakuwaza kuwa yeye atafikaje kule na ataishije kule bali kuendelea kupambana ili afike kule.

Lakini Wathesalonike inatukumbusha kuhusu kazi za mikono yetu, kwenye mkono sisi tuweke miguu kwa heshma la andiko hili kwa watoto wadogo wasioelewa lugha ya picha, tunahitaji masimulizi ya kazi za miguu yake pale Morocco?? Au tuweke nukta kisha tupate maji.

Kwa heshma ya Msuva nikaona kuna haja ya kupitia Wathesalonike, niliposikia kuhusu urejeo wa Farid Mussa, nilipokumbushwa stori za Shaibu Ninja, nilipotupiwa karatasi la Haruna Moshi kuondoka Gefle IF iliyoshiriki UEFA, nilikaa pembeni na kalamu yangu kusoma vyema sura hii iliyoandikwa miaka 500 kabla ya Kristo.

Nikipata muda nitamsomea Msuva kitabu cha “THE SPY WHO LOVED FIDEL CASTRO” mikono ya Nathaliz Ortega, niliupenda sana ukurasa wa 15-17, HAKIKA NITAMSIMULIA.


UMEJARIBU HII POKER YA VIDEO?

Jaribu sasa hapa Meridianbet. Ukiacha ukweli kuwa itakupa burudani maridadi, bado inakuhakikishia ushindi mkubwa. Kazi kwako kukusanya ushindi!

Meridianbet Casino

INGIA MCHEZONI!

18 Komentara

    Habari njema

    Jibu

    kabisa wakati ukifika kila kitu kinakuwa safi kabisa kikubwa subira

    Jibu

    Subra ndo kila kitu

    Jibu

    Muda ukifika Kila kitu uwa sawa!!

    Jibu

    Hbaari njema hii msuva yupo vizuri

    Jibu

    Msuva yupo vizuri

    Jibu

    Kijana namkubali sana

    Jibu

    Msuva yupo vzr sana

    Jibu

    Wakati ukifika kila kitu kitakuwa sawa

    Jibu

    Msuva anajuaaa

    Jibu

    Msuva yupo vizuri sana

    Jibu

    Msuva mtu mbaya

    Jibu

    Safii Sana Msuva namkubali Sana nimtu asiye katatamaa kiungo huyo anapambana ili afikie anapo pataka jembe huyo kwaiyo subila umpa mtu manufaa ya kimchezo kwaiyo Msuva akiyake kufanya kitu kinacho stairi nakutufanyia kitu chakutupendeza sisi mashabiki

    Jibu

    Msuva yupo vizuri

    Jibu

    Msuva kama msuvaaa fundi

    Jibu

    Asnt kwa taarif meridianbet

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Kila la kheri Msuva

    Jibu

Acha ujumbe