Wasiwasi umetawala kwa wapenzi wa Liverpool baada ya taarifa za jeraha la Joe Gomez, ambaye anaripotiwa huenda akawa na jeraha sawa na la lile linalomuweka Van Dijk nje ya dimba.

Nyota huyu mwenye miaka 23 ameenda kufanyiwa vipimo kujua hali ya jeraha lake, lakini ripoti ya awali inawapa hofu wana-Liverpool.

Kama ikiwa ripoti kamili baada ya uchunguzi itathibitisha ukubwa wa jeraha la Joe Gomez katika kiwango ambacho kinahofiwa basi itakuwa ni taarifa mbaya sana kwa Liverpool.

Liverpool tayari wameshampoteza Van Dijk kwa sehemu ya msimu iliyosalia, ni wazi kuwa hawapo katika nafasi ya kumpoteza tena mchezaji kama Gomez kwa wakati huu.

Van Dijk alipata jeraha katika Debi ya Merseyside na amefanyiwa upasuaji mapema mwezi huu. Wakati huo Trent Alexander Arnorld naye anatarajiwa atatumia takribani mwezi mzima kuuguza jeraha lake.

Thiago Alcantara na Alex Oxlade-Chamberlain pia hawapo dimbani. Huu ni mtihani, bila shaka Guardiola anaandaa namna bora ya kuushinda.


UMEJARIBU HII POKER YA VIDEO?

Jaribu sasa hapa Meridianbet. Ukiacha ukweli kuwa itakupa burudani maridadi, bado inakuhakikishia ushindi mkubwa. Kazi kwako kukusanya ushindi!

Meridianbet Casino

INGIA MCHEZONI!

19 MAONI

  1. majeraha yamekuwa ndo changamoto kubwa sana kwa wachezaji wengi na iyo inatokana na kukaa kipindi kirefu bila mazoezi sababu ya gonjwa la corona

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa