US Open Final: Raducanu vs Fernandez

Ni ukweli usiopingika, unaposikia mchezo wa tenesi, unafikiria majina kama Naomi Osaka na Serena Williams. Safari hii, fainali ya US Open imekuja na majina mapya!

Wakati dunia ikiendelea kutafuta suluhisho la muda mrefu la kuendana na maambukizi ya Covid 19, sekta ya michezo ni miongoni mwa sekta zilizoathiriwa kwa kiasi kikubwa. Vivyo hivyo, baadhi ya wanamichezo wameshindwa kuendelea na shughuli zao kutokana na sababu mbalimbali zinazohusiana na Covid19.

Emma Raducanu

US Open ni miongoni mwa mashindano makubwa kwenye ulimwengu wa tenesi na michezo kwa ujumla. Hakika, 2021 imekua ya namna yake. Sio Naomi Osaka, Serena Williams, Ashleigh Barty wala Zabalenka aliyetinga fainali.

Vijana wadogo – Emma Raducanu(Uingereza) na Leylah Fernandez(Canada), wameruka visiki vingi na vikubwa mpaka kufika hatua ya fainali.

US Open
Leylah Fernandez

Raducanu (miaka 18) anakua mcheza tenesi wa kwanza (mwanamke) kutoka Uingereza kucheza fainali ya US Open kwa miaka 53 iliyopita. Ushindi wa seti 6-1 6-4  dhidi ya Maria Sakkari unampeleka kijana huyu fainali yake ya kwanza ya Grand Slams.

Fernandez (miaka 19) alimshinda Aryna Sabalenka kwa seti 7-6 (7-3) 4-6 6-4 ikiwa ni muendelezo wa kuwashinda vigogo akiwemo Naomi Osaka na Elina Svitolina.

Mchezo wa fainali ya US Open 2021 (wanawake) utachezwa jumamosi hii ambapo vijana hawa watauonesha ulimwengu namna nyota zao zinavyong’aa.


USHINDI KIGANJANI KWAKO!

Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.

Meridianbet Online Casino

INGIA MCHEZONI HAPA

Acha ujumbe