Tetesi zinasema, Everton watafikiria uwezekano wa kocha wa Rangers Steven Gerrard na kocha wake wa zamani wa Liverpool Rafael Benitez kuchukua nafasi ya Carlo Ancelotti.

Pia kocha wa zamani wa Wolves Nuno Espirito Santo yuko kwenye orodha ya Everton ya uwezekano wa kuwa kocha wao mpya.

Mchezaji wa zamani wa safu ya ulinzi wa Liverpool Jamie Carragher anaamini kuwa kocha wa zamani wa klabu hiyo Rafa Benitez ni chaguo bora kuchukua nafasi hiyo huko Goodison park.

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 33, yuko karibu kukubali mkataba wa miaka miwili kusalia Barcelona.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Arsenal wanaongoza kwenye mbio za kumpata winga wa Manchester City Muingereza Raheem Sterling, 26, mpango ambao unaweza kumzuia mshambuliaji Harry Kane, 27, kujiunga na City akitokea Tottenham.

Manchester United wanakabiliwa na ushindani katika kumnasa mlinzi wa Sevilla Jules Kounde kwani Barcelona pia ina mpango wa kumsajili mchezaji huyo raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22.

Tetesi zinasema, Arsenal wanajiandaa kukamilisha taratibu za kumsajili mlinda lango wa Cameroon Andre Onana, 25, kutoka Ajax, kwa pauni milioni 1.7.

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich binafsi ana mpango wa kumchukua mshambuliaji wa Ubelgiji anayekipiga Inter Milan Romelu Lukaku , 28, kumrejesha klabuni.

Tetesi zinasema Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel atapatiwa mpaka pauni milioni 200 kwa ajili ya matumizi ya msimu huu wa kiangazi.

Tetesi zinasema Kiungo wa kati wa Barcelona Miralem Pjanic, 31, anataka kurejea Juventus.

Tetesi zinasema Kocha mpya wa Roma Jose Mourinho anatazamia kumsajili mlinda lango wa AC Milan, Muitaliano Gianluigi Donnarumma, 22.

 

Gianluigi Donnarumma

Mpango wa Leicester City kwa ajili ya kiungo wa kati wa Lille Boubakary Soumare, 22, unaweza kukamilika haraka kuliko ilivyodhaniwa baada ya klabu hiyo kuondolewa katika michuano ya Euro.

Tetesi zinasema Manchester United wanamtolea macho kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Pedro Goncalves, 22.

Leeds United itatafuta mbadala baada ya kushindwa bei ya kumpata beki wa kushoto wa Ufaransa Romain Perraud, 23.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa