Tetesi zinasema, Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba, 28, alimpuuza kocha Ole Gunnar Solskjaer baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika kichapo cha 5-0 dhidi ya Liverpool Jumapili na mfaransa huyo amesimamisha mazungumzo ya mkataba mpya wa kusalia klabuni hapo.
Tetesi zinasema, Newcastle wako tayari kumpa Ten Hag mshahara wa £6m kwa mwaka baada ya kodi na kufanya marupurupu yote kufikia £11m kwa mwaka lakini Mholanzi huyo, 51, amegoma kuondoka Ajax.

Meneja wa zamani wa Roma Paulo Fonseca, 48, anatarajia kukubali ofa ya kuwa Meneja mpya wa Newcastle, lakini wamiliki wapya wa klabu hiyo bado wanatafakari uamuzi wao.
Tetesi zinasema, Barcelona bado wanamatumini ya kumpata kocha wa Liverpool Mjerumani Jurgen Klopp, 54, ili amrithi kocha wa sasa Ronald Koeman.
Arsenal inahaha kumshawishi William Saliba kwamba maisha yake ya soka ni pale Emirates na wanaweza kulazimika kumuuza mlinzi huyo mfaransa, 20, ambaye ameonyesha kiwango cha kuvutia Marseille anapocheza kwa mkopo.
Tetesi zinasema, Arsenal wanajiandaa kupambana na Manchester City katika mbio za kumsajili kama mchezaji huru mlinzi wa Hispania Sergi Roberto, 29 kutoka Barcelona.
Kiungo wa Manchester United, Donny van de Beek amemkataa wakala Mino Raiola baada ya wakala huyo kumuomba mholanzi huyo mwenye miaka 24 awe wakala wake mpya.

Chelsea imepewa ofa ya kumsajili mlinzi wa Uholanzi mwenye miaka 22 Matthijs de Ligt wakati huu Juventus ikitaka kupunguza kiwango cha mishahara inayotoa kwa wachezaji.
Tetesi zinasema, Aston Villa, AC Milan na Bayer Leverkusen ni miongoni mwa vilabu vinavyomtaka mshambuliaji wa River Plate Muargentina Julian Alvarez, 21.
Barcelona imemfahamisha winga wake Mfaransa Ousmane Dembele, 24, kwamba ana mwezi mmoja tu wa kukubali ofa yao mpya ya kuongeza mkataba wake wa sasa ambao unakoma mwishoni mwa msimu ujao.
Mchongo wa mkwanja mrefu kutoka kasino bora za mtandaoni za Meridianbet. Mchezo wa Circus Fever unakuweka katika nafasi nzuri ya kuwa mshindi. Furahia kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa meridianbettz.

CHEZA HAPA

