Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Real Madrid haitajaribu kumsajili Kylian Mbappe, 22 mwezi Januari badala yake itatupa ndoano kwa mshambuliaji katika dirisha lijalo la kiangazi -mkataba wake na Paris St-Germain utakapotamatika.

Tetesi zinasema, Kiungo mchezeshaji Mbrazil Philippe Coutinho, 29, atawakacha Newcastle United mwezi Januari kwakua hana mpango wa kuondoka Barcelona.

Wolves wako tayari kumuuza winga wa Hispania Adama Traore mwezi Januari wakati huu mazungumzo kuhusu mkataba mpya yakiendelea kusuasua, na klabu yake ya zamani Barcelona itachuana na Liverpool kuwania saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 25.

 

Kocha wa zamani wa Chelsea Frank Lampard anataka kurejea ligi kuu England msimu huu akiifuatilia Leicester City iwapo Brendan Rodgers ataondoka kwenda kurithi mikoba ya Ole Gunnar Solskjaer pale Manchester United.

Wayne Rooney anatarajia kusalia kama kocha wa Derby County licha ya ” the Rams” kukatwa alama 9 zaidi na kusalia shimoni kushuka daraja baada ya kukubali kuvunja sheria za fedha.

Real Madrid huenda ikatupa ndoano zake kwa kiungo wa Manchester United Muholanzi Donny van de Beek katika dirisha la mwezi Januari wakati huo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24.

 

Karim Adeyemi

Barcelona inajiandaa kuipa Red Bull Salzburg kitita cha £33.8m kwa ajili ya kumsajili Karim Adeyemi – lakini Borussia Dortmund wako kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumsajili mshambuliaji huyo Mjerumani mwenye miaka 19.

Burnley wako tayari nyota wake James Tarkowski amalizie mkataba wake msimu ujao kuliko kumuuza mwezi Januari – huku West Ham na Newcastle wakimtaka mlinzi huyo wa kati wa England, 28.

Tetesi zinasema, Everton huenda ikatoa £5m kumsajili Calum Chambers, 26, mwezi Januari kama watashindwa kumpata kwa mkopo mlinzi mwezie wa Arsenal Ainsley Maitland-Niles, 24.

 

Dean Smith

Tetesi zinasema, Meneja mpya wa Norwich City Dean Smith anapanga kuungana tena na kiungo wa Aston Villa kutoka Jamhuri ya Ireland, Conor Hourihane, 30, mwezi Januari.

Kiungo wa Uholanzi Xavi Simons atafikiria kuondoka Paris St-Germain wakati mkataba wake itakapomalizika msimu ujao, huku vilabu vya Hispania na Ujerumani wakimfuatilia kinda huyo mwenye miaka 18.

Tetesi zinasema, Nottingham Forest wanamtaka mlinzi wa kati wa Hearts na Scotland John Souttar, 25, na wana matumaini ya kuibwaga Rangers kwenye mbio za kupata saini yake mwezi Januari.

Borussia Monchengladbach na Crystal Palace zinamuwania mshambuliaji wa Arsenal Eddie Nketiah, 23 ambaye anataka kuondoka mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu.


WIKI NJEMA NA CRAZY TIME CASINO!

Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.