Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Liverpool itafanya mazungumzo na Fulham mwezi huu kuhusu mkataba kwaajili ya mshambuliaji mwenye umri wa miaka 19 Fabio Carvalho, huku wakitaka kufikia makubaliano kabla ya msimu ujao.

Manchester United wanafuatilia mwenendo wa mlinzi wa Chelsea Antonio Rudiger akiripotiwa kukataa ofa ya hivi karibuni ya mkataba wa klabu hiyo, mkataba wa thamani ya karibu pauni laki 200 kwa wiki.

 

Rudiger

Liverpool wanamfuatilia kwa karibu mchezaji wa klabu ya Le Havre mwenye umri wa miaka 17 Andy Elysee Logbo ambaye alikuwa analinganishwa na mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku.

Mshambuliaji wa West Ham, Michail Antonio ameitaka klabu hiyo kuboresha kikosi chake cha mashambulizi na kusaini mkataba na mshambuliaji mwingine msimu huu.

Tetesi zinasema, Mkurugezi wa AC Milan Paolo Maldini ameweka wazi mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, 40, atasaini mkataba mpya katika klabu.

Tetesi za Arsenal kumtaka mchezaji wa Paris Saint-Germain Georginio Wijnaldum, 31, zimejitokeza tena baada ya kiungo huyo wa kati kuachwa nje ya kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya mechi yao ijayo ya Championi Ligi dhidi ya Real Madrid.

 

Liverpool

Watford wamejaribu kumsajili mlinzi Phil Jones mwenye umri wa miaka 29- kutoka Manchester United lakini hawakufanikisha kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho katika mwezi wa Januari.

Barcelona wakishindwa kumsajili Erling Braut Haaland, 21, msimu huu wamemlenga Alexander Isak, 22, kutoka klabu ya Real Sociedad, na Antony, 21, wa Ajax , au Lisandro Martinez, 24.

Tetesi zinasema, Manchester United wanajiandaa kutuma ofa ya kumnunua Araujo, ambaye mkataba wake wa Barcelona unamalizika 2023.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.