Tetesi zinasema, Manchester City imepata nguvu katika mbio zao za kumshawishi mshambuliaji wa Inter Milan Muargentina Lautaro Martinez, 24 Inter inaripotiwa kumtaka mshambuliaji wa Monchengladbach, Marcus Thuram, 24, kuziba nafasi yake.

Tetesi zinasema, Roman Abramovich tayari amepokea ofa kadhaa zinazokaribia dau la £3bn za kuinunua Chelsea.

Barcelona inatarajiwa kumsajili kiungo wa Wolves Ruben Neves katika majira ya joto, huku mazungumzo kati ya wawakilishi yakielezwa kufanyika. Manchester United na Arsenal pia zimeonyesha nia ya kumtaka mreno huyo mwenye miaka 24 wanaomuhusudu kwa muda mrefu.

 

Solskjaer Amgeukia Neves wa Wolves.

Tetesi zinasema, Aston Villa inawataka kiungo wa AC Milan Franck Kessie, 25, na mshambuliaji wa Atletico Madrid, Luis Suarez, 35, katika dirisha lijalo la usajili la majira ya joto.

Chelsea imempa ofa ya mwisho kujaribu kumbakisha Christensen pale Stamford Bridge, huku mlinzi huyo wa kimataifa wa Denmark akitajwa kukaribia kusaini mkataba wa awali kujiunga na Barcelona kwenye dirisha lijalo la usajili.

Tetesi zinasema, Villa italazimika kulipa £21m kwa ajili ya kiungo wa Paris St-Germain Georginio Wijnaldum, 31.

Tetesi zinasema, Kiungo wa England Jude Bellingham, 18, ameamua kusalia Borussia Dortmund angalau kwa msimu mwingine mmoja.

Tetesi zinasema, AC Milan imeripotiwa imefikia makubaliano na mlinzi wa Lille muholanzi mweye miaka 22, Sven Botman baada ya kukataa kujiunga na Newcastle United.

 

Botman

Mkurugenzi wa michezo wa PSG Leonardo amefunga mjadala wa tetesi kwamba Kylian Mbappe ataondoka kujiunga na Real Madrid au Liverpool, akisema mfaransa huyo mwenye miaka 23 amepewa mkataba mpya mnono.

Kocha wa Barcelona Xavi Hernandez ameelekea ujerumani kukutana na mshambuliaji wa Borussia Dortmund striker Erling Haaland kujaribu kushinda mbio za kumsajili Mnorway huyo mwenye miaka 21.

Juventus inajiandaa kuvunja mkataba wa Aaron Ramsey, 31 katika majira ya joto baada ya Rangers kusema hawatarajii kumsajili moja kwa moja kiungo huyo wa Wales anayechezea hapo kwa mkopo mwishoni mwa msimu.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa