Tetesi zinasema, Manchester United wamemwambia kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 25, kwamba wataelekeza mawazo yao kwingine kama hatoweza kuamua kama anataka kuja Old Trafford msimu huu wa joto.

Tetesi zinasema, Manchester United, Liverpool, Arsenal na Chelsea wote wanamtaka Tchouameni na watakuwa tayari kuingilia kati ikiwa uhamisho wake kwenda Madrid hautafanikiwa.

Tetesi zinasema, AC Milan wanataka kumfunga mshambuliaji wa Ureno Rafael Leao, 22, kwa mkataba mpya wa kukataa nia ya Real Madrid.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Mshambulizi wa Everton Richarlison, 25, anaweza kuondoka Goodison Park msimu huu wa joto huku Tottenham, Real Madrid na Paris St-Germain zikimhitaji mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil.

Everton inachuana na West Ham kumsajili mshambuliaji wa Burnley na Ivory Coast Maxwel Cornet, 25, baada ya Clarets kushushwa daraja kutoka Ligi ya Premia.

Inter Milan watamsajili Henrikh Mkhitaryan, 33, mkataba wake wa sasa na Roma utakapokamilika msimu wa joto. Kiungo huyo wa Armenia pia anafikiria ofa kutoka kwa washindi wa Ligi ya Europa Conference.

Tetesi zinasema, Arsenal wanavutiwa na kiungo wa Lens Cheick Doucoure, 22. Hata hivyo, Brighton, Everton, Crystal Palace na Wolves pia wanamfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Mali.

Manchester United wanaweza kuwasilisha ofa kwa Christopher Nkunku anayelengwa na Liverpool na Chelsea wiki ijayo, huku mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 akisita kusaini mkataba mpya na RB Lepizig.

 

Barca

Paris St-Germain haitamsajili winga wa Barcelona Ousmane Dembele, 25, msimu huu wa joto licha ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kuhusishwa pakubwa na kurejea katika nchi yake.

Manchester United pia wamefanya mazungumzo ya ndani na meneja mpya Erik ten Hag kuhusu beki wa Ajax na Uholanzi Jurrien Timber, 20, na beki wa kati wa Villareal kutoka Uhispania Pau Torres, 25.

Tetesi zinasema, West Ham itasikiliza ofa kwa kiungo wa Jamhuri ya Czech Tomas Soucek, 27, msimu huu wa joto kufuatia kuripotiwa kutofautiana na meneja David Moyes.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa